Maonyesho ya ajira sekta ya Afya kwa halmashauri ya mkoa wa Mwanza na nyinginezo yamefanyika wilayani sengerema mkoani Mwanza.
Lengo ni kuwatambulisha wanafunzi wa sekta ya Afya kuhusu nafasi za kazi zilizopo katika Halmashauri ya mkoa wa Mwanza ambapo maafisa ajira toka Halmashauri zote walikusanyika wilayani hapa na kuziainisha nafasi zilizopo kwenye wilaya zao.mfano Wataalam wa maabara, wauguzi, katibu afya na nyinginezo.
Katibu Tawala Msaidizi - Utawala na Utumishi Crecensia Joseph akitoa hotuba ya ufunguzi.
Monitoring and Evaluation Oficer wa Benjamin Mkapa HIV AIDS Foundation Desderi Wengaa akitoa maelezo kuhusiana na kusudio la Taasisi hiyo kuziainisha nafasi za ajira sekta ya Afya.
Wadau hao wa Sekta ya Afya walipata fursa ya kuandika majina yao kwa wilaya walizotaka kufanya kazi pamoja na anuwani, mawasiliano ili pindi mchakato utakapo kamilika waitwe kwaajili ya kufanya kazi.
Katibu wa Afya Wilaya ya Geita akitoa maelezo na vivutio vilivyopo toka wilaya yake.
Katibu wa Ukerewe Ester Marick akitoa maelezo ya nafasi za ajira na vivutio vilivyopo katika halmashauri hiyo.
No comments:
Post a Comment