Baadhi ya wakazi wa Bonde la Jangwani Jijini Dar wakiwa katika hali ya kuhamisha vitu vyao mara baada ya eneo la makazi yao kujaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.Inasemekana kuna watu kadhaa wamepoteza maisha kutokana na kuzidiwa na maji hayo.
Hawa nao mambo hata hayajawaendea vyema maana wao ndio wamezungungukwa na maji kila kona.
Mali zikiondolewa.
Hapa hata kwa kupita hakuna,maji yamejaa kila kona.
Jamaa akiwa amembeba mdogo wake wakati akimvusha kwenye eneo hilo lililokuwa limejaa maji yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo huku pembeni yao kukiwa na Mkokoteni uliokuwa umebeba takataka ambao ulikwama kwenye maji hayo.
Hawa jamaa wa huku kama wakitaka kufika barabarani basi ni lazima watumia mtumbwi ama ngalawa maana upande wao unamaji mengi ambayo ni ya kupiga mbizi.
Hakuna shughuli inayofanyika leo katika eneo hili la Bonde la Jangwani,maana maji ni kila kona.
Baadhi ya wakazi wa Eneo hilo la Bonde la Jangwani wakiwa ni wenye huzuni kutokana na nyumba zao kujaa maji na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
No comments:
Post a Comment