Meneje huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Bi Tunu Kavishe
akikabidhi moja kati ya Cherejani nne kwa Mwenyekiti chama cha UVIMA
(toka shoto) Bi Tatu Ngao pamoja na Katibu wake Asha Mbelwa wa kata
ya Mpiji Majohe karibu na PUGU nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
ikiwa ni msaada wa Airtel kwa Vikundi hivyo vinavyohusika na kusaidia
na kuwezesha jamii zenye uhitaji vilivyopo chini ya usimamizi wa Mke
wa Raisi Mama Salama Kikwete. UVIMA ni Umoja wa Vikundi vilivyo chini
ya WAMA. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi za UVIMA
zilizopo Majohe
Meneje huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Bi Tunu Kavishe
akikabidhi moja kati ya Baiskeli nne kwa Mwenyekiti wa chama cha UVIMA
(toka shoto) Bi Tatu Ngao pamoja na Katibu wake Asha Mbelwa wa kata
ya Mpiji Majohe karibu na PUGU nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
ikiwa ni msaada wa Airtel kwa Vikundi hivyo vinavyohusika na kusaidia
na kuwezesha jamii zenye uhitaji vilivyopo chini ya usimamizi wa Mke
wa Raisi Mama Salama Kikwete. UVIMA ni Umoja wa Vikundi vilivyo chini
ya WAMA. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi za UVIMA
zilizopo Majohe.
Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel imewasaidia wakina mama wa
kikundi cha UVIMA cha Mpiji Majohe kilichopo PUGU nje kidogo ya jiji
la Dar Es Salaam kwa kuwapatia msaada wa Cherehani nne pamoja na
Baiskeli nne ili zitumike kusaidia kuanzisha shule ya Ushonaji kwa
manufaa ya kikundi hicho.
Wakizungumza katika hafla ya kupokea misaada ya baiskeli nne pamoja na
vyerehani vinne kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Airtel wanawake
wa kikundi cha UVIMA yaani Umoja wa Vikundi Vilivyo Chini ya WAMA
kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika mtaa wa MPIJI
MAJOHE uliopo PUGU DSM wamesema misaada ya namna hiyo imekuwa
ikisaidia pia kukuza pato la Taifa.
Leo hii misaada kama hii tunayoipata inasaidia sana sisi wakina mama
wa UVIMA kuweza kuzalisha chakula na hatimae tutawasaidia watoto
yatima waliopo mtaani kwetu na kwenye baadhi ya nyumba za wana
kikundi, pia wajane pamoja na watu wenye uhitaji maalum alisema Bi
Tatu Ngao Mwenyekiti wa UVIMA kata ya MAJOHE
Tunatoa ahadi kwa kampuni ya Airtel waje waone msaada waliotupatia leo
baada ya miezi sita tutakuwa tumefanya mambo makubwa na mazuri zaidi
aliendelea kusema Bi Tatu Ngao.
Kwa upande wake meneja huduma kwa jamii wa AIRTEL, Bi. Tunu Kavishe
amesema AIRTEL itaendelea kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali
ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ujenzi wa Taifa.
Airtel Tanzania Tulifahamu UVIMA kupitia WAMA na walitueleza jinsi
UVIMA ilivyo na matarajio makubwa hivyo na sisi airtel tukaamua kutoa
mchango wetu huu ili kuwezesha dhamira yenu yakusaidia wajane, watu
wenye virusi vya ukimwi, wazee pamoja na Watoto yatima alisema Bi Tunu
Kavishe Meneja Huduma kwa Jamii Airtel.
Airtel bado tunaendelea na mkakati wa kuhakikisha tunasaidia jamii
kupitia sehemu zote muhimu ili kupunguza matatizo ya jamii ambayo pia
nasisi tunaitegemea kuendelea kufanya Biashara yetu
Mwakani tutaendelea kujitoa katika mambo muhimu ikiwemo Elimu pamoja
na Afya ya jamii ili tuwe na wateja na jamii ya uhakika
zaidi.alimaliza kusema Bi Tunu.
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa ikitoa misaada ya aina mbalimbali
katika jamii ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika huduma za jamii.
Vikundi vya UVIMA yaani Umoja wa Vikundi Vilivyo Chini ya WAMA viko
chini ya Uangaliazi wa Mama Kikwete na dhamira yake kuu ni kusaidia
wakina mama, watoto yatima, jamii yenye virusi vya ukimwi, wajane
pamoja na familia zenye uhitaji maalum kwa kuwapatia misaada na mbinu
mbalimbali za kujikwamua.
No comments:
Post a Comment