HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 3, 2011

wanahabari wapata fursa ya kuangalia kipindi cha Guinness football challange 2011 kupitia kituo cha televisheni cha itv

Meneja wa kinywaji cha Guinness,Morris Njowoka (pili kulia) akielezea na  kuonyesha kwenye I-pad  jinsi mywanji wa bia ya Guinness anavyotakiwa kuinywa,wakati wa hafla fupi ya wanahabari (hawapo pichani) waliofika kwenye hafla hiyo fupi ya kushuhudia kipindi cha Guinness Football Challange 2011,kinachorushwa na televisheni ya ITV,kila siku ya jumatano kuanzai saa tatu usiku,hafla hiyo ilifanyika jana usiku kwenye ufukwe wa Cine Club,jijini Dar. wengine pichani ni wadau wanaotangaza kinywaji hicho.
Baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini wakifatilia kwa makini kipindi cha Guinness Football Challange 2011 (GFC) kilichokuwa kikirushwa na kituo cha televisheni cha ITV.Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd,(SBL) ,kupitia kinywaji chake cha Guinness,jana jioni iliandaa hafla fupi kwa waandishi wa habari za Michezo kushuhudia kipindi cha Guinness Football Challange 2011 (GFC),ambapo jana kipindi hicho kilikuwa hewani ikiwa ni sehemu ya nne, ambapo Tanzania walifanikiwa kuingia robo fainali na kufanikiwa kujinyakulia zawadi ya dola 6,000,Aidha katika shindano hilo,mshindi anakuwa na nafasi ya kuibuka na zawadi ya dola 50,000 za Kimarekani.
Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Mwananchi,Michael Matemanga akionesha ujuzi wake wa kupiga dana dana,kwenye hafla fupi ya kutazama kipindi cha Guinness Footbal Challange 2011,iliyofanyika kwenye ufukwe wa Cine Club,jijini Dar.Wanahabari mbalimbali walialikwa kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad