HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 23, 2011

Wabunge wa CPA Tawi la Tanzania wamtembelea Balozi Sefue

Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania ambao ni viongozi wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) tawi la Tanzania walipomtembelea Ofisini kwake New York, Marekani wakiwa njiani kuelekea Dominica, West Indies kwa ziara ya mafunzo, pichani kutoka kushoto ni Mhe. John Paul Shibuda, Mb wa Maswa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CPA Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu,Mbunge wa Ilala na Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania, Mhe. Lucy Owenya, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CPA ya Tanzania na Nd. Saidi Yakubu, Katibu wa Msafara huo na Afisa Mratibu wa Masuala ya Jumuiya ya Madola Bungeni
Balozi Ombeni Sefue katika mazungumzo na Waheshimiwa Wabunge Ofisini kwake.
Wabunge wa Tanzania wakitembelea jengo la Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa lililonunuliwa hivi karibuni ambapo Ubalozi huo unatarajia kuhamia, wa pili kulia ni Mama Rose Mkapa, Afisa Utawala wa Ubalozi huo.
Mama Rose Mkapa akitoa maelezo kwa wabunge wanaomsikiliza kwa makini walipotembelea moja ya ofisi zilizoko katika jengo hilo lenye ghorofa sita ambalo Ofisi ya Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa inatarajia kuhamia na pia kutoa fursa kwa wapangaji wengine kupangisha ndani ya jengo hilo.Wabunge hao walitembelea jengo hilo kujionea wenyewe ikiwa pia ni sehemu ya kazi zao kama wawakilishi wa wananchi hususan Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mb na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mhe. John Paul Shibuda,Mb ambae ni Mjumbe wa Kamati hiyo.Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad