Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi (katikati) akianzisha mbio za Bendera ya Taifa Za Kili Mjini Dodoma ambapo aliwaaga wanariadha 30 wanaokimbiza bendera hiyo kuelekea Moshi kupitia Kampeni ya Jivunie uTanzania inayoenda sambamba na miaka 50 ya Uhuru kwa udhamini wa Bia ya KIlimanjaro Premium Lager.
Wanariadha 30 wanaokimbiza Bendera ya Taifa ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Kili Jivunie uTanzania inayoenda sambamba na sherehe za miaka 50 ya Uhuru wakianza mbio hizo Mjini Dodoma jana kuelekea Moshi. Mbio hizi zimedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Wanariadha wengine wameanzia Mwanza na wa Dar es Salaam wanaondoka leo.
No comments:
Post a Comment