Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Scania Tanzania,Mark Cameron akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,kuhusiana na Mashindano ya Kumtafuta Dereva Bora wa Mwaka nchini Tanzania ambayo yatafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza tarehe 19/11/2011 katika viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Scania Tanzania,Godwin Rwegasira akifafanua jambo wakati wa kutangaza Mashindano ya kumtafuta Dereva Bora wa Mwaka yanayotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Scania Tanzania,Mark Cameron.
Logo ya Mashindano hayo kwa mwaka huu.
Mashindano ya kumtafuta dereve bora wa Mwaka ,yaliyoanzishwa barani ulaya na kampuni ya Magari ya Scania mwaka 2003, na baadaye kuenea katika nchi mbalimbali barani ulaya kwa lengo la kutambua umuhimu wa dereva,yameanzishwa nchini kwa mara ya kwanza na kampuni hiyo ikiwa na lengo la kumtambua dereva na kutambua mchango wake na katika jamii,ujuzi na taaluma ya dereva barabarani
Ikiwa ni moja ya kampuni kubwa ya kutengeneza malori na mabasi duniani , Scania imeonyesha wajibu na majukumu yake katika suala zima la usalama barabarani. Na kwa kufanikisha hilo Scania imekuwa ikitoa mafunzo kwa madereva ili kumfanya awe makini wakati wote anapokuwa barabarani,hivyo ndio maana imefikia uamuzi wake wa kuanzisha mashindano hayo ambayo yataonyesha umuhimu wa madereva nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo,Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Scania Tanzania , Mark Cameron alisema kuwa “ dereva ni mtu muhimu sana katika kuimarisha uchumi, kulinda mazingira pamoja na usalama kiujumla”
Madereva wenye ujuzi na ufanisi barabarani, huongeza uzalishaji, hupunguza majanga barabarabi na kuchangia usalama barabarani kwa wakati wote.
Kampuni ya Scania nchini Tanzania, itazinduwa kwa mara ya kwanza “mashindano hayo ya kumtafuta dereva bora wa mwaka Tanzania” yatakayo fanyika tarehe 19/11/2011 katika viwanja vya Biafra vilivyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
“Mashindano ya kumtafuta dereva bora wa mwaka nchini Tanzania” yanatoa fursa bora kwa kujadili na kushugulikia masuala ya ajali za barabarani ili kusaidia kuondoa tatizo hilo na hatimaye kuongeza faida endelevu ndani ya kampuni na kwa jamii nzima .Pia kampuni ya Scania inaadhimisha ujuzi wa dereva na kuonesha mchango wao muhimu katika jamii hususani kwa vijana wenye fani hiyo.
Ndugu Cameron aliongeza kuwa, “Madereva ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji Mashindano ya kumtafuta dereva bora wa kitanzania kwa mwaka huu, ni mwanzo wa mashindano menginena yatakayo kuwa na msisimko zaidi kwa madereva wengine na yataongeza ufanisi na umakini wa madereva barabarani. Mashindano hayo yatakuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili.
Mshindi katika mashindano hayo atajinyakulia kitika cha sh. mil. 5 pamoja na kwenya kushiriki mashindano ya bara la Afrika yatakayofanyika nchini Afrika ya kusini.
No comments:
Post a Comment