HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 10, 2011

Cpwaa atajwa kuwa Balozi wa Kili katika Kampeni ya Jivunie uTanzania

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akikabidhi fungu la udhamini kwa msanii wa muziki wa Bongo Flava Juma Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa aliyechaguliwa kushindania tuzo za Channel O za Video bora ya Muziki kutoka Afrika Mashariki. Cpwaa alitangazwa kuwa Balozi wa Kili manjaro katika Kampeni ya Jivunie uTanzania.

Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imemtangaza msanii nyota wa muziki wa Bongo Flava, Juma Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa kuwa Balozi wa Bia hiyo hususani katika Kampeni inayoendelea ya Kili Jivunie uTanzania kama sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru.

Hili limebainishwa wakati wa makabidhiano ya tiketi mbili za kusafiri Afrika Kusini kwa hisani ya Kilimanjaro Premium Lager baada ya msanii Cpwaa kuchaguliwa kuwania Tuzo za Video za Channel O. Washindi wa tuzo hizo watatangazwa Ijumaa Novemba 11, 2011 Mjini Sandton, Johannesburg.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema kampuni yake inajivunia kujihusisha na msanii huyo kama njia ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio.

“Akirudi Cpwaa atasaidia katika shughuli mbalimbali za Kili hususan Kampeni inayoendelea ya Jivunie uTanzania,” alisema.

Cpwaa alishinda tuzo mbili wakati wa Tuzo za Muziki Tanzania za mwaka 200/10 na za mwaka huu, 2010/2011 ambapo alishinda katika kundi la video bora ya mwaka. Tuzo hizi zinadhaminiwa na Kilimanjaro premium Lager.

Video ya wimbo wake wa action ambao ulimpa tuzo katika Tanzania Music Awards ndio uliofanya achaguliwe kuwania tuzo ya Chanel O mwaka huu.

Cpwaa ameongozana na Meneja wake Juma Adam Mikidadi, Muongozaji wa video, Luciano Gadie Tsere na maprodyuza wawili wa video. Msanii huyo atatumia safari hii kurekodi video yake mpya.

Kwa upande wake Cpwaa alisema,” Naishukuru sana Kilimanjaro premium Lager kwa msaada huu na hii inadhihirisha wazi nia yake ya kufikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio.”

Aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Kilimanjaro ili kufanikisha Kampeni yake ya Jivunie uTanzania.

Kampeni hii ilizinduliwa rasmu mwezi Julai mwaka huu kama sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru lengo kuu ikiwa kuwakumbusha Watanzania walikotoka, walipo sasa na wanakokwenda na kikubwa zaidi kuwakumbusha wajivunie mafanikio yakiyopatikana ndani ya miaka 50 ya Uhuru.

Kili inaendelea kufanya tamasha mbalimbali katika mikoa mbalimbali nchini na kilele cha kamppeni hii kitakuwa kupandisha bendera ya Tanzania juu ya Mlima Kilimanjaro siku chache kabla ya sherehe za kitaifa Disemba 9.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad