HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 4, 2011

Unakumbuka wimbo wa Eddy Sheggy ulioitwa Shakaza??Hebu jikumbushe kidogo


Na John Kitime
Jambo ambalo naliona wazi ni kuwa Watanzania wanapenda sana nyimbo za dansi zinazotokana na nyimbo zenye asili ya makabila ya hapa Tanzania. 

Nikikumbuka nyimbo kama Mtaulage, Malaine, Nyongise, ambazo ni kazi yangu mwenyewe nikiwa Tancut na Vijana Jazz, kila Munu ave na kwao ya Les Mwenge, Boko wa Kilimanjaro Band, Shakaza ya Bantu na nyingi nyingine zote zilichukua nafasi ya juu katika anga za muziki wakati wake, na hata sasa. 
Pengine lingekuwa somo kwa wanamuziki wa Tanzania na kuliangalia hili katika tungo zao. Hebu tumkumbuke Eddy Sheggy hapa akiwa na Bantu, akiimba na ndugu zaki Francis na Christian.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad