HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 25, 2011

SAFARI LAGER YATANGAZA UDHAMINI WA TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA POOL KWENYE MASHINDANO YA ALL AFRICA CUP 2011 - BLANTYRE- MALAWI


Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa Pool,Denis Lungu akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi cha kitakachoshiriki mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011 yatakayofanyika mjini Blantyre nchini Malawi kuanzia Novemba 22-26,2011.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscer Shelukindo na kulia ni Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza kwa mara nyingine kuidhamini timu ya Taifa katika mashindano ya ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI yanayotarajiwa kuanza tarehe 22.11.2011 mpaka 26.11.2011.


Akitangaza udhamini huo, Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo alisema “Bia ya Safari lager imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imekuwa ikiidhamini timu ya Taifa ya mchezo wa pool table tangu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Africa na Dunia.

Naye kocha mkuu wa timu ya taifa, Denis Lungu alitangaza majina yafuatayo ya timu ya taifa inayotarajia kuingia kambini tarehe 29.10.2011 kujiandaa na mashindano hayo.

TEAM A
1 OMARY AKIDA - KINONDONI
2 FELIX ATANAS- DODOMA
3 GODFREY MHANDO- KINONDONI
4 MOHAMED IDDY- KINONDONI
5 ALLY AKBAR- TEMEKE

TEAM B
1 BONIFACE JOHN- ARUSHA
2 BARAKA JOAKIM- MBEYA
3 JOGORY MAKENZI- MWANZA
4 ANTONY THOMAS- ILALA
5 RAMADHANI ALLY- MOROGORO
6 EMMANUEL LOYA-DODOMA
7 SHAMIS NASSORO- ILALA
8 CHARLES VENAS- TMK
9 ABDALLAH HUSEIN- KINONDONI
10 EMMANUEL SANKA- MANYARA

Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya ALL AFRICA CUP yanatajiwa kushirikisha nchi 14 wanachama wa ALL AFRICA POOL ASSOCIATION (AAPA) na nchi hizo ni Africa kusini, Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Cameroon, Zambia, Uganda, Swazland, Reunion FFB, Reunion Arabas, Nigeria , Msumbiji, Kivinjari chako huenda kisiauni kuonekana kwa picha hii. Morocco na Kivinjari chako huenda kisiauni kuonekana kwa picha hii. Lesotho.

Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema “ Mchezo wa pool table sasa umekuwa si mchezo tena wa kupoteza muda bali ni mchezo kama michezo mingine na unaelekea kuwa ajira rasmi kwa vijana wa Tanzania. 

Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuiweka Tanzania katika ramani ya michezo kimataifa kupitia SAFARI LAGER BEER ni fahari kubwa kwa mchezo wa pool table Tanzania. 

TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad