Meneja wa Kinywaji cha Redd’s,Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati akitangaza kufanyika kwa tamasha la kwanza kwa wabunifu na wanamitindo wa vyuo vya Dar es Salaam la “Redd’s Uni-Fashion Bash” ,litakalofanyika kesho jumamosi kwenye ukumbi wa FPA Uliopo Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.kushoto ni mmoja wa washiriki wa Tamasha hilo.
Meneja wa Kinywaji cha Redd’s,Victoria Kimaro (kushoto) akisalimiana na washiriki wa tamasha hilo leo.
Kinywaji cha Redd’s Original kinachotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kesho kitafanya tamasha lake la kwanza kwa wabunifu na wanamitindo wa vyuo vya Dar es Salaam. Tamasha hili lijulikanalo kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” lililozinduliwa mwanzoni mwa mwezi Oktoba likiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya wabunifu na wanamitindo walioko katika vyuo vya elimu ya juu.
Akizungumzia tamasha hilo linalotarajiwa kuwa la kipekee na lenye mvuto mkubwa, meneja wa kinywaji cha Redd’s,Victoria Kimaro alisema "Kesho (Jumamosi) tarehe 29, ndiyo ile siku tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu kubwa. Tutakuwa na fainali za tamasha la Redd’s Uni – Fashion Bash kwa vyuo wa Dar es Salaam litakalofanyika katika ukumbi wa FPA Uliopo chuo kikuu cha Dar Es Salaam karibu na Benk ya CRDB (Udsm) hapa Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni na kuendelea".
"Maandalizi yote ya tamasha hili ambalo limeandaliwa kwa umakini wa hali ya juu ili kuonesha utofauti na matamasha yaliyozoeleka yemeshakamilika, na tutakuwa na washiriki kumi katika nyanja ya ubunifu (designers) watakoonesha kazi zao, pia tutakuwa na wanamitindo (models) ishirini watakao vaa mavazi ya wabunifu hao na kupita nayo jukwaani.
Redd’s Original pia imeandaa burudani za kutosha ili kunogesha tamasha hilo, ambapo wasanii Roma Mkatoliki na John Makini watatoa burudani ya kutosha, pia nawakumbusha wanavyuo wote kuwa tamasha hili halina kiingilio, hivyo ni ruksa kwa vyuo vyote vya hapa Dar es Salaam kuja kushuhudia vipaji vya wanavyuo wenzao na kupata burudani", alisema Bi. Victoria.
Akizitaja zawadi za washindi Bi Kimaro alisema; Redd’s Original pia itatoa zawadi kwa washindi kama ifuatavyo;
WABUNIFU
MSHINDI WA KWANZA 700,000
MSHINDI WA PILI 500,000
MSHINDI WA TATU 300,000
MSHINDI WA NNE NA WA TANO 100,000 KILA MMOJA
WANAMITINDO
MSHINDI WA KWANZA 500,000
MSHINDI WA PILI 400,000
MSHINDI WA TATU 300,000
MSHINDI WA NNE NA WA TANO 100,000 KILA MMOJA
Wasiriki walioingia fainali kwa mkoa wa Dar Es Salaam ni. 1.Aloycia Innocent (USSM)2.Rosemary Osward (CBE).3.Magreth Mhoza (MNMA.4.)Upendo Kuboja(CBE)
5.Kudra Lupatu (CBE)6.Emmanuel Elly (CBE).7.Lameck Stephen (IFM)
8.Benson Macha(CBE) 9.Saadat Juma Saadat (IFM)10.Conrad Gumbo(IFM)11.Issack Ibrahim(UDSM)12.Amos Kalinga(UDSM)13Asha Mohamed(KIU)14.Rose Hubert
(KIU)15Gerald Kalinga(UDSM)16.Hussein Kasimu(UDSM)17.Happyness Mushi(CBE)
18.Yalita Malanduzi(UDSM)19.Brian Abdul(CBE)20.Rosa Damazo(IFM) na majaji wa fainali hizi watakuwa 1.Taji Liundi 2.Farouk Abdala,3.Hamissa Hassan 4.Castantine Magavile.
Matamasha haya pia yatafanyika katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza na Dodoma mapema mwezi Novemba. Kinywaji cha Redd’s Original kimekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia ya urembo, ubunifu na mitindo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment