Mmoja wa waandishi wa habari wa michezo akijibu swali aliloulizwa na Mwalimu wa waandishi wa habari ambae ni mkufunzi Said Salim,katika semina ya kuwanoa waandishi wa habari za michezo wanaoshiriki semina hiyo iliyoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mjini Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari za michezo wakiwa katika semina ya kuwanoa waandishi wa habari za michezo iliyoandaliwa na Taswa na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Mjini Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro
Joel Bendera amewataka waandishi wa habari za michezo kuacha dhana
potofu ya kuripoti habari za uchochezi na badala yake waripoti zile
habari zinazoelimisha jamii kwa ujumla.
Bendera
alitoa kauli hiyo wakati wa semina ya waandishi wa habari za michezo
waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari za
michezo nchini TASWA yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mkuu huyo alisema kumekuwa na huruka ya waandishi wengi kupenda kuripoti habari za migogoro jambo ambalo linachochea migogoro na kupelekea kushusha taaluma ya michezo hapa nchini.
Hali kadhalika hali hiyo imetolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Kilosa, Halima Dendego ambaye alifunga mafunzo hayo
yaliyoshirikisha jumla ya waandishi 40 kutoka mikoa ya Pwani, Morogoro
na Dar es Salaam, chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano Vodacom Tanzania.
Akizungumza
na Waandishi wakati akifunga mafunzo hayo alisema waandishi wa michezo
pia wanatakiwa kuacha ushabiki wa Simba na Yanga kitendo ambacho kinachangia kupotosha sekta nzima ya uandishi wa habari za michezo.
‘’Nawaomba mzingatie mafunzo mliopata ili kuboresha zaidi sekta ya habari za michezo,” alisema Dendego.
Alisema TASWA imefanya jambo la muhimu kuandaa mafunzo hayo kitendo ambacho kimetoa changamoto kwa wanahabari kuripoti habari znye usahihi tofauti na vyo saa wmekuwa wakiripoti habari za ushabkzaidi
Aliongeza kusema si kila siku mnaegemea kuandika migogoro na habari ambazo hazina tija kwa jamii ya wanamichezo wa Tanzania mnatakiwa kuandika habari ya uhakika kutokana na kwamba waandishi ni kioo cha jamii..
Alisema
kutokana na mafunzo hayo, waandishi hao watakuwa wamekwiva vya kutosha
na matunda yake anayategemea kuyaona watakavyorejea katika vyombo vyao
vya habari.
Aliongeza
kwa kuwashukuru wadhamini wa mafunzo hayo, kampuni ya simu za mkononi
Vodacom na wadhamini washiriki kampuni ya mabasi ya Al Saedy Bus Service kwa kujitolea kudhamini mafunzo hayo.
Ameahidi pia, kushirikiana na TASWA bega kwa bega katika kuendeleza michezo nchini, kwa sababu kuna mingine kama Mpira wavu na netiboli imedorora.
Kwa upande wa Vodacom kupitia Meneja Uhusiano na habari za Mtandao, Matina Nkurlu alisema, kutokana
na kampuni hiyo, kwa muda mrefu imekuwa mdau muhimu katika kuendeleza
sekta ya michezo Kitaifa na Kimataifa nchini haikusita kudhamini mafunzo
hayo.
‘’Vodacom imekuwa ikidhamini michezo
mbalimbali, kama Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Vodacom Miss
Tanzania, Mwanza Cycle Challenge , Kilimanjaro Marathon na Mashindano ya
mbio za mashua za Vodacom Regata, imekuwa ikidhamini pia mafunzo ya kunoa waandishi wa habari kama ilivyofanya, alisema Matina.
Aliongeza
kuwa: ‘’Pamoja na kufanya biashara bado tunaona ni muhimu kutoa mchango
katika hii ili kuiwezesha Tanzania siku moja kuwa moja ya nchi
zinazofanya vizuri kwenye michezo kama tunavyosikia majina ya nchji za Nigeria, Ghana, Afrika Kusini na nyingine.’’
No comments:
Post a Comment