Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sam Ellangallor
|
Airtel Tanzania imetangaza gharama mpya za kupiga simu Kenya na Uganda. Kupitia punguzo hilo wateja wa Airtel ndugu na jamaa zao sasa wataweza kufanya biashara kwa urahizi hasa zile zinazohusisha kuvuka mipaka ya nchi yetu na kuhusisha nchi za Kenya au Uganda kwa punguzo nafuu sana la Tsh 2.50 tu badala y sh 5 na sent 16
“Huu ni muendelezo wa kati ya dhamira endelevu tulizonazo Airtel kuwapa unafuu hasa wafanya biashara kuweza kufanikisha mahusiano yao kibiashara kati ya nchi moja hadi nyingine”
Akisisitizia Dhamira hiyo ya kupunguza gharama za mawasiliano kwa simu za kwenda nje ya nchi Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sam Ellangallor aliendelea kusema “Airtel ni mtandao pekee unaotoa mawasiliano yenye uhakika zaidi kwa nchi za afrika mashariki. Airtel bado tutaendelea kuongoza kwa kutoa mawasiliano bora na kwa gharama nafuu zaidi tukiwa tunalengo thabiti la kuondoa kabisa changamoto ya mawasiliano katika nchi za Afika Mashariki”
Maendeleo ya uchumi wa jamii huwezeshwa na muunganiko wa jitihada au nyenzo nyingi, hivyo ninaimani kuwa kuvuka kwetu mpaka na kurahisisha mawasiliano ni dhairi itasaidia kukuza na kuboresha maisha ya jamii zote. Hili imewezeshwa zaidi na wateja wanaendelea kujiunga kila siku pamoja na dhamira yetu ya kutendelea kusambaa nchi za jirani” aliongeza kusema, Sam
No comments:
Post a Comment