Toka Kulia ni Afisa Biashara wa Airtel Arusha Bi Monica Ernest akikabidhi msaada wa vitabu kwa Wanafunzi wa shule ya Ngarenaro (toka shoto) . Neema Asenga na Christina daudi wakati mgeni Rasmi Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa (kati) akishuhudia. Airtel imekabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne vitakavyogawanywa katika shule za Olorien sekondari, Themi Sekondari, Sinoni Sekondari pamoja na Ngarenaro.makabidhiano hayo yaifanyika katika shule ya sekondari Ngarenaro Arusha. Mwishoni mwa wiki
Toka Kulia ni Afisa Biashara wa Airtel Arusha Bi Monica Ernest akikabidhi msaada wa vitabu kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Ngarenaro Ramadhan Mshana wakati mgeni Rasmi Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa (kati) akishuhudia. Airtel imekabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne vitakavyogawanywa katika shule za Olorien sekondari, Themi Sekondari, Sinoni Sekondari pamoja na Ngarenaro.makabidhiano hayo yaifanyika katika shule ya sekondari Ngarenaro Arusha. Mwishoni mwa wiki
Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Airtel bw, Stephen Iketi Akyoo akikabidhi msaada wa vitabu kwa mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari ya Ngarenaro Bi. Eva Mlingi mbele ya mgeni Rasmi Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa (kati) akishuhudia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyoandaliwa na Airtel katika shule ya Ngarenaro. Airtel kupitia mpango wako wa Shule yetu imekabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni nne vitakavyogawanywa katika shule za Olorien sekondari, Themi Sekondari, Sinoni Sekondari na pamoja na Ngarenaro. Mwishoni mwa wiki
Kampuni ya simu za mkoni Airtel imekabidhi msaada wa vitabu kwa shule nne zilizoko mkoani Arusha
Akikabidhi
msaada Meneja wa Airtel kanda ya Kaskazini Stephen Akyoo alisema “Kanda
yetu ya Kaskazini tunajuimuisha mikoa ya Manyara,Arusha,Kilimanjaro na Tanga. Tayari tumeshagawa Tanga wiki iliyopita leo Arusha na wiki ijayo tunaenda manyara
Katika kutambuwa umuhimu na mahitaji ya jamii yetu,Airtel ilianzisha mpango unaoitwa SHULE YETU wenye
lengo la kuinua kiwango cha elimu nchini. Chini ya mpango huu shule
mbalimbali za sekondari nchini zinaendelea kupata vitabu vya kiada na
ziada vyenye thamani ya shilling milion moja kwa kila shule. Tangu tulipoanza mpango huu tumeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zaidi ya 800 Tanzania bara na visiwani na kugawa vitabu vyenye thamani zaidi ya shilingi billion moja.
Shule zitakazopokea msaada huu wa vitabu ni Ngarenaro, Themi, Sinoni na Oloirieni sekondari zilizopo mkoani Arusha.
Kwa niaba ya kampuni ya Airtel napenda kutoa shukurani za dhati kwa ushirikiano tunaoupata kwa uongozi wa Mkoa na Mashule kwa ujumla.
Akipokea msaada huo Afisa Elimu Manispaa ya Arusha kwa shule za sekondari Bi. Violet Mlowosa alisema “napenda kuishukuru sanaAirtel kwa kuikumbuka jamii ya Arusha
Msaada
huu hakika ulikuwa unahitajika sana na utasaidia kuboresha elimu katika
shule hizi. Hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani Airtel inathamini elimu
na nimatumaini yangu wanafunzi wetu watasoma kwa bidii na kupata elimu
iliyo bora.
Wote
mnaelewa kwamba Serikali ina mzigo mkubwa sana na inaweka kila juhudi
kuboresha sekta ya elimu nchini. Tunahitaji misaada kutoka kwa
wafanyabiashara ili kutimiza malengo tuliyojiwekea. Nawashukuru sana
Airtel kwa kusaidia juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu
nchini na kusaidia watoto wetu kupata elimu nzuri.
Jina
“ shule yetu” sio geni katika masikio yetu, na Airtel wanasema
wamechagua kujenga Taifa kupitia sekta ya elimu. Mchango huu wa Airtel
ni ishara tosha ya nia yao thabiti ya kusaidia elimu nchini. Na Serikali
kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatambua mchango wa
Airtel katika sekta ya elimu kwa kipindi cha miaka saba mfululizo sasa.
Wote
tunaelewa Elimu ni msingi wa familia na Taifa thabiti. Elimu huwapa
vijana wetu fursa ya kufanikiwa siku za usoni na kufanya maamuzi ya
busara katika maisha yao ya kila siku. Nawashukuru Airtel kwa mchango
wenu na kuwaomba makumpuni mengine kusaidia sekta ya elimu ili kujenga
taifa lililo bora.
No comments:
Post a Comment