Mzee Kipara enzi zake wakati bado ana
nguvu
Mzee Kipara akijaribu kushuka kitandani
Akisaidiwa kusimama na wageni
waliokwenda kumjulia hali
Napenda
nitoe masikitiko yangu kwa wasanii wa Sanaa ya Maigizo
wote Nchini kwa kutoonyesha msimamo
wa pamoja ili kuweza kumsaidia Mzee wetu Mzee Kipara (Fundi Said) ambaye kwa
sasa ana afya ambayo sio nzuri pamoja na uzee
lakini hali ngumu ya
kimaisha ndio inayochangia zaidi.
Mzee
Kipara ni
msanii wa muda mrefu sana katika
Tasnia hii ya
sanaa
ya Uigizaji, ni muigizaji mkongwe sana
katika Taifa letu, kwa wale wasiomjua alianza kuigiza sanaa toka mnamo mwa
miaka ya
1964 enz za RTD (Redio Tanzania) kwa sasa TBC hii kwa
faida ya
vizazi vya sasa msio fahamu hili.
Baadae Mzee kipara walianzisha kikundi cha maigizo
ambacho kikawa kinarushwa na kituo cha ITV ambacho amedumu nacho kwa
muda mrefu sana kikiitwa Kaole.
Katika kipindi chote hiki cha Kaole
aliwafundisha wasanii wengi sana ambao kwa sasa
wengi mnawasikia au mnaziona kazi zao kwenye Luninga
zenu.
Cha kunisikitisha wengi wao
hawajaonyesha upendo wao hata kidogo kwa mzee huyu, nitakua
mnyimi wa Fadhila kama sita mshukuru sana Stephen Kanumba nakumbuka alikua
msanii wa kwanza kwanza kwenda
kumsaidia huyu Mzee; namshukuru sana, najua wapo wengine ambao pia walikwenda
kwa nyakati tofauti tofauti kuweza
kumuona huyu mzee au hata kumsaidia kwa chochote
kile.
Mimi binafsi kama mwakilishi wa
KAPINGAZ Blog napenda
kuwashukuru wote waliofanya hivyo, ila ombi langu
kwenu ninyi wasanii wa sanaa ya
Maigizo ni kwa nini
msiandae tamasha lolote ambalo mnaweza mkakusanya kiasi
kikubwa cha fedha kikaweza kumsaidia huyu Mzee wenu badala ya kwenda
mmoja mmoja kumuona huyu Mzee, kumbukeni na nyie ni
vijana kwa leo itafika wakati mtazeeka kama huyu mzee na watatokea
wengine mmewafundisha hiyo sanaa naamini na nyie mnaweza mkasikitika
kama mzee huyu.
Naomba
niwape mfano wa Dada Asha Baraka, Mkurugenzi wa African Star
(Twanga Pepeta) nampongeza sana huyu dada aliweza kuandaa tamasha la Dansi kwa
ajili ya
kukusanya michango ya
kumsaidia Mzee Muhidin Ngurumo ili aweze kupata matibabu vizuri, na mpaka
leo naandika masikitiko yangu, Mzee Ngurumo leo anapanda
kwenye stage kuimba na wenzie katka tamasha la sikukuu ya Idd el
Fitr.
Nawaomba wasanii wote katika sanaa ya maigizo
muweze kulitazama hili la Mzee Kipara kama ni jambo lenu wote, na
hata mnapokua mnakwenda kwenye vikao vyenu na BASATA muweze kuliongelea hili,
ili muweze kua na umoja wenye nguvu wa kuweza kusaidiana kwenye matatizo kama
haya.
Tunawaona mara kwa mara mnaenda kufanya shughuli mbali mbali sehemu
tofauti, hasa za kujipongeza katika mafanikio flani ni
vema mnapokua huko mkumbushane la mzee huyu msimuache aishi maisha
haya ni aibu
kwenu wasanii wote hasa zaidi nyie
mliopitia Kaole.
Naomba wana Blog wenzangu tushirikiane katika
hili. Asante
mimi naongezea hata wasio wasanii pia tumsaidie mzee kipara ufanyike utaratibu ikiwa kwa njia ya bank au njia nyengine. chochote mtu alichokuwa nacho achangie au mnalionaje hili wadau wenzangu?? mdau Leicester.uk.
ReplyDelete