HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 10, 2011

Ufugaji wa Kuku

Mtaalam wa mitambo ya kutotolesha vifaranga aliyetokea Shirika la Elimu Kibaha Isdori Chikawe akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Kampuni ya RRS Family Enterprises ‘Fuga Ufaidike’ JACQUELINE CHIPANDA (Wa kwanza kulia) ufanyaji kazi wa mitambo hiyo. Kwa wiki kampuni hiyo inazalisha vifaranga 30,000. Mwingine ni mfanyakazi wakiwana hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya RRS Family Enterprises ‘Fuga Ufaidike’ Sumbuko Chipanda ya jijini Dar es Salaam ambayo inayojihusisha na utotoleshaji wa vifaranga aina ya ROSS 308 kutoka Marekani akionesha mayai yaliyo kwenye mtambo tayari kwa kutotoleshwa.
Mtaalam wa mitambo ya kutotolesha mayai aliyetokea Shirika la Elimu Kibaha Isdori Chikawe akimuelekeza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya RRS Family Enterprises ‘Fuga Ufaidike’ Sumbuko Chipanda ya jijini Dar es Salaam ambayo inayojihusisha na utotoleshaji wa vifaranga aina ya ROSS 308 kutoka Marekani jinsi mitambo hiyo inavyofanya kazi.
Wataalam wa mitambo ya kutotolesha vifaranga aina ya Ross 308 yanayoingizwa kutoka Marekani wakipanga maboksi ya vifaranga tayari kwa matumizi. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya RRS Family Enterprises ‘Fuga Ufaidike’ Sumbuko Chipanda ya jijini Dar es Salaam inayoingiza mayai hayo.

Na Mwandishi Wetu

Watanzania nchini wametakiwa kujikita kwenye ufugaji wa kuku ili wajikomboe kwenye umaskini unaowakabili hususani kwenye maeneo ya vijijini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya RRS Family Enterprises inayojihusisha na utotoleshaji wa vifaranga aina ya ROSS 308 Jacqueline Chipanda amesema wafugaji wengi wamejikwamua kwenye umaskini baada ya kujiingiza kwenye ufugaji wa kuku.

Akifafanua Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa wafugaji wanaozingatia ufugaji wa kisasa huku wakitumia vifaranga bora aina Ross 308 ambavyo mayai yake yanaingizwa kutoka Marekani ni wazi wafaidika kama ilivyo kauli mbiu yao ‘Fuga Ufaidike’.

Amesema biashara hiyo inawezwa kufanywa na mtu hata mwenye uwezo mdogo wa kuweza kufuga kuku hata mia moja tofauti na miradi mingine ambapo mtaji unatakiwa uwe mkubwa.

“Kama nilivyosema mradi huu unaweza kufanywa hata na mjasiriamali mdogo wa kipato cha chini. Ukuaji mzuri wa kuku unategemeana na aina ya mfugaji anayezingatia dawa za kuulia wadudu na chakula,” alisema Chipanda.

Kampuni hiyo inayoendesha shughuli hizo za utotoleshaji vifaranga vya kuku ina mashine 12 zenye uwezo wa kuzalisha vifaranga 30,000 kila wiki ambapo kila Jumamosi na Jumapili vifaranga hivyo vimekuwa vikipatikana.

Akizungumzia suala la ubora wa vifaranga aina ya Ross 308 Chipanda amesema kabla ya kuagiza mayai yake kutokea Marekani huzingatia ripoti yake ili kubaini kama yana madhara kwa mlaji wa Kitanzania.

Vilevile alisema awali walikuwa wakiagiza mayai hata kutoka nchi za Asia lakini baada ya kutokea hatari ya homa ya mafua ya ndege nchi hizo zilizuiwa na sasa wanaingiza bidhaa hiyo kutoka Marekani.

Kuhusiana na ufugaji bora na wa kisasa Mkurugenzi huyo wa RRS Family Enterprises ‘Fuga Ufaidike’ amesema, wanatoa pia mafunzo ya ufugaji kuku katika shamba lao lililopo Mbezi Mwisho ambapo vifaranga hivyo vinapatikana pia.

Takwimu nchini zinaonesha kuwa mahitaji ya mazao ya kuku yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kuwapo walaji wengi wa nyama na mayai yatokanayo na kuku wa asili na kisasa.

Tanzania inaelezwa kuwa na kuku wa asili milioni 34 wanaofugwa, milioni 20 wa kisasa, bata milioni 1.2, bata mzinga 900,000 na kanga 400,000.

Kwa upande wa uzalishaji wa kuku wa mayai umeendelea kuongezeka pia, kwani kwa mwaka 2005/06 pekee kulikuwa na vifaranga milioni 26.8 vya kuku wa biashara, ambavyo vilizalishwa nchini na vingine milioni 2.1 vilivyoagizwa kutoka nje.

Alisema mayai ya kutotoa vifaranga milioni 8.4 yaliagizwa kutoka nje na kuwa uzalishaji wa mayai uliongezeka kutoka bilioni 1.8 mwaka 2005/06 huku ulaji wa mayai kwa mtu kwa mwaka ukiongezeka kwa asilimia 20.7 kutoka 53 hadi 64.

Takwimu hizi zinaashiria umuhimu wa kuku nchini kama hatutakuwa makini kuzuia na kuwakinga kuku hawa na maradhi kama mafua ya ndege, wananchi wengi wataathirika kiuchumi,” amesema Chipanda.

2 comments:

  1. Mimi ninayo mashine ya kutotosha mayai ina uwezo wa kutotoa vifaranga 1056 ni mpya haijawahi kutumika inauzwa wasiliana na namba 0715 009952

    ReplyDelete

Post Bottom Ad