Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa, akiwapa maji watoto kutoka vituo vya kulelea watoto ya tima vilivyopo katika jimbo lake alipo vialika nyumbani kwake kushiriki katika futari pamoja naye jijini Dar es Salaam jana.
Mmoja wa wanachama wa kikundi cha wajasiriamali wenye ulemavu cha Mvuti jijini Dar es Salaam Dotto Mshoro, akimkabidhi unga wa muhogo wnaozalisha kwenye kikundi Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa, mara baada ya kufuturu nao nyumbani kwake ukonga jana.
Baadhi ya maustaadhi walioalikwa katika futari ya muheshimiwa mbunge wa jimbo la ukonga Eugene Mwaiposa aliyoiandaa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam jana.
Na Francis Dande
WATANZANIA wametakiwa kuwa na moyo wakujitolea kwa kuwawezesha wasiokuwa na uwezo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza umasikini wa kipato kwa wanachi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wenye ulemavu wa viungo kutoka Mvuti nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam,Salum Naida wakati walipoalikwa nyumbani kwa Mbunge wa jimbo la Ukonga kushirikiana naye katika kufuturu.
Naida alisema kuwa nivizuri watanzania wenye uwezo wakalenga zaidi katika kuwawezesha watu wa makundi maalumu kama walemavu yatima na wajane kuliko kuwapa misaada midogo midogo ambayo haiwasaidii sana.
“Tunamshukuru sana huyu mbunge kwani mimi nina umri wa miaka 40 na ni mlemavu tangu enzi hizo lakini sijapatapo kufika nyumbani kwa kiongozi hata mmoja lakini huyu ana moyo wapeke yake tuna mshukuru sana, amekuwa karibu na sisi na anatusaidia sana kwenye kikundi chetu kila mara,” alisema.
Futari hiyo ambayo ilijumuisha watu wenye ulemavu watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wajane kutoka vituo mbalimbali jimboni humo wapatao 200.
Nae mama mlezi wa kituo cha kulea watoto waishio katika mazingira magumu Uyaweko Women group cha Gongo la Mboto Mary Katobesi, alimshukuru mbunge huyo na kusema kuwa katika kipindi cha miaka 10 tangu kituo hicho kuanzishwa hawajawahi kualikwa nyumbani kwa mbunge yeyote kwahiyo wamefurahi kupata fursa hiyo.
Kituo hicho ambacho pia kinalea watoto wapatao 340 huku kikishirikisha na wajane katika harakati zake za kupambana na hali ngumu ya maisha.
Nae Mbunge huyo alitoa wito kwa jamii kujitahidi kuonyesha ushirikiano katika shida na raha kwa wengine ambao kwa namna moja ama nyingine wanaonekana hawana uwezo ili kuleta usawa katika jamii.
No comments:
Post a Comment