HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 5, 2011

maonyesho ya nanenane mkoani Dodoma leo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, David Mathayo David wakikagua ufugaji wa kuku wa nyama na mayai wa kisasa wakati walipotembelea banda la Balton Tanzania Limited kwenye maonyesho ya Nanenane, Nzuguni, Dodoma leo.
Ng'ombe mwenye jina la Mkapa Nzagamba akiongozwa na mmiliki wake, Mashishanga kutoka Nkasi mkoani Rukwa katika mashindano ya mifugo Kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nanenane, Nzuguni,Dodoma leo. Mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, David Mathayo David wakitazama ng'ombe wa kisasa wa maziwa katika mashindano ya kitaifa ya mifugo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nanenane, Nzuguni Mjini Dodoma.
Afisa Elimu na Mazingira kutoka Ofiisi ya Makamu wa Rais, Bw. Daniel Sagata (kushoto) akitoa maelezo kuhusu suala la Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kwa mkazi wa Dodoma ,Bw. Vob De Graar katika viwanja vya nanenane Nzuguni mjini Dodoma ambapo maonyesho ya wakulima yanafanyijka Kitaifa mjini hupo.
Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais,Bw Charles Swai (kushoto) akitoa maelelezo kwa mwananchi wa Dodoma kuhusu masuala ya Mazingira katika viwanja vya Nanenane Nzuguni mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad