HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 30, 2011

Airtel yafuturisha wateja wake - Mwanza

Afisa mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kanda ya ziwa, Galus Mgawe akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake wa makampuni katika Hoteli ya Golden Krest , Mwanza juzi.
Baadhi ya wateja wa Airtel wa makampuni wakifuru wakati wa FUTARI iliyoandaliwa na Airtel maalum kwa baadhi ya wateja wa makampuni katika Hoteli ya Gold Crest, Mwanza jana.

Kampuniya simu za mkononi ya Airtel imewafuturisha baadhi ya wateja wake wa Mwanza ikiwa ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja wake walioko kila mahalia.

Akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja katika Hoteli ya Golden Krest jijini Mwanza Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa , Bw Galus Mgawe alisema “ tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii.

Airtel huwa tunakutana na wateja wetu katika maswala mbali mbali ya jamii ikiwemo michezo burudani na hata katika kuinua sekta mbali mbali mfano afya na elimu,

Lakini leo ni siku muhimu kwetu Mwanza kwa kuwa tunafuturu pamoja na kutakiana mfungo mwema wa ramadhani na pia tutaitumia fursa hii kutakiana sikukuu njema ya Iddi ambayo imekaribia.

Ahadi yetu kwa wateja wote ni kwamba bado Airtel tutaendelea kuboresha huduma zetu ili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa pamoja na kutoa mawasiliano kwa gharama nafuu kushinda yote. Alimaliza kwa kusema Bw Galus Mgawe

Nae afisa Uhusinao wa Airtel Tanzania Bi, Jane Matinde kwa niaba ya Airtel aliwatakia wateja wote mfungo mwema wa Ramadhani pamoja na maandalizi mema ya sikukuu ya iddi inayokuja

“Airtel tunawatakia mfungo mwema wa ramadhani lakini pia maandalizi mema ya sikukuu!, endeleeeni kufurahia sms 100 za bure baada ya kutuma smsm 4 tu, pia furahieni huduma bora za barua pepe pamoja na kupiga simu katika kutakiana sikukuu njema kila mahali” aliema Bi Matinde

Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.Bado Airtel inampango wa kutoa misaada katika mikoa ya mbalimbali kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad