Mchezaji wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni,Ibrahim Abeid akipiga mpira katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya ya Taifa ya Safari Lager uliopigwa mchana wa leo kwenye ukumbi wa Kilimani Club,mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Ilala,Rahim Mohammed akifanya vitu vyake katika mchezo wa robo fainali.
Mchezaji wa timu ya Pool mkoa wa Arusha,Bashir Hamis akipiga mpira wakati wa mchezo wake dhidi ya Elias Manjere wa timu ya mkoa wa Kilimanjaro.
Aloyce Zacharia wa timu ya mkoa wa Kagera akiusikilizia mpira alioupiga kuona kama utaingia kwenye shimo ama vipi wakati wa mchezo wa hatua ya mchezaji mmoja mmoja katika mashindani ya Pool ya Taifa ya Safari Lager yanayoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa Kilimani Club,mjini Dodoma.
Mwanadada Judith Machafuko wa timu ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni,akionyesha umahiri wake wa hali ya juu katika mchezo wake dhidi ya Mwanadada Mwenzie,Rukia Issa kutoka mkoani Mwanza.katika mchezo huu,Judith aliibuka kidedea kwa ushindi wa kishindo.
Mashindano yakiendelea vyema kabisa huku kila timu ikionyesha umahiri wake.
No comments:
Post a Comment