HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 11, 2011

Makamu wa raisi azungumzia muitikio wa Kudhibiti UKIMWI Tanznaia

  Makamu wa Rais ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mohammed Gharib Bilal  

Na Glory Mziray -New York
Makamu wa rais ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mohammed Gharib Bilal amesema Tanzania ni kati ya Nchi zilizofanikiwa kujizatiti katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutahadharisha kuwa tusibweteke na mafanikio tuliyopata ila tuendeleze vita hii ili kufikia malengo ya milenia.

Makamu wa rais amesema Mkakati mpya wa ulimwengu wa kutokomeza UKIMWI kwa mpango wa sifuri 3 ambazo ni maambukizi mapya sifuri, vifo vya magonjwa yanayohusiana na UKIMWI sifuri na unyanyapaa sifuri unaenda sambamba na kaulimbiu ya Tanzania bila UKIMWI Inawezekana na Mpango wa Tanzania kuanzisha mfuko wa UKIMWI ili kukidhi mahitaji ya afua za udhibiti na kufikia Lengo hilo na kwa kufanya hivyo tunakuwa tumejibu mpango wa milenia lengo namba 3,4, na 5 ambao unataka mama mjamzito na mtoto kupata huduma zote za afya zinazohitajika.

Akijibu swali la mtangazaji wa radio UN bi Florah Nducha aliyetaka kufahamu mpango wa dawa unavyoleta ahueni na hivyo kusababisha maambukizi zaidi Makamu wa Rais amesema dawa inafubaza makali ya virusi vya UKIMWI hivyo kupunguza kasi ya kuambukiza ukilinganisha na mgonjwa aambaye hatumii dawa.

akifafanua zaidi kuhusu dawa Makamu wa Rais amesema ushirikiano uliopo na nchi wanachama wa Umoja wa mataifa umetoa mwanga zaidi kwa nchi zilizoendelea kuonesha nia ya kutengeneza dawa za aina ya kupunguza makali(generic) ili kuwezesha watu wote kupata tiba kila inapohitajika na kwa asilimia mia moja.Amezitaja nchi hizo kuwa ni Brazil, India na Thailand.

Akizungumza awali Bw. michele Sedibe, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia UKIMWI amesema haitavumilika kuona watu wa baadhi ya Nchi wanapata dawa zenye madhara mengi wakati baadhi ya nchi wanapata dawa zenye madhara machache au zisizo na madhara kabisa.

akizungumzia kuwasaidia wanawake kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI mh. makamu wa rais amesema tafiti mbalimbali za masuala ya kuwasaidia wanawake zinaendelea na Tanznaia ina nafasi bado ya kutumia kukinga maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto njia ambayo mpaka sasa inatumika kwa asilimia 53 tu japokuwa tuna nafasi ya kutumia kwa asilimia 100 .

kauli hii imeungwa mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia UKIMWI- UNAIDS Bw. michele Sedibe ambaye alisema watoto 400,000 wanazaliwa na virsi vya UKIMWI kila mwaka bara la africa wakati mabara mengine hakuna mtoto anayezaliwa na virusi vya UKIMWI.

nia ya Makamu wa rais ya kuwasaidia wanawake katika kudhibiti UKIMWI inaenda sambamba na ari iliyotolewa na Katibu wa Umoja wa Mataifa alipokuwa akifungua mkutano wa wake za marais alisema wanawake wakiumwa tunapoteza silaha nambari moja inayotupatia chakula kwa watoto na familia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad