HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFANYA MAHOJIANO NA MTANGAZAJI WA UN REDIO NEW YORK

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya viongozi wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati akishiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi unaofanyikajijini New York jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisalimiana na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN) Flora Nducha, wakati mtangazaji huyo alipofika kwa ajili ya kufanya mahojiano naye kuhusu maudhui ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi uliofanyika jijini New York, na unatarajiwa kumalizika Juni 10, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), Flora Nducha, muda mfupi baada ya kuhudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu masuala ya ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaofanyika jijini New York
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na mshauri Mkuu wa ufundi na Asasi ya Viongozi wa Afrika inayohusika na vita dhidi ya Malaria, Dkt. Melanie Renshaw (wa pili kulia) na Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue (kulia) na Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa inayohusika na vita dhidi ya Malaria, Saleemah Abdul-Ghafur (kushoto), wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Tacaids, Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) na Mkurugenzi wa Tume ya Ukimwi Zanzibar, Dkt. Omari Shauri (kulia) wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad