Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Edith Mushi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza rasmi kufanyika kwa tamasha kubwa la kukabidhi Tuzo na fedha kwa washindi wa Tuzo za GrandMalt Exellence Award 2011 kwa vyuo vya elimu ya juu jijini Dar.Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Matl,Consolata Adam
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisichokuwa na kilevi cha GrandMalt inatangaza rasmi kufanyika kwa tamasha kubwa la kukabidhi Tuzo na fedha kwa washindi wa Tuzo za GrandMalt Exellence Award 2011 kwa vyuo vya UDSM.ARDHI,IFM,CBE,DUCE na USTAWI WA JAMII..
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Meneja wa kinywaji cha GrandMalt nchini Bi Consolata Adam alisema TBL kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha GrandMalt kiliandaa Tuzo za kutambua michango na juhudi binafsi zinazofanywa na wanachuo wa elimu ya juu nchini Tanzania.
Alisema tuzo hizo zinatambulika kwa jina la Excel with GrandMalt awards 2011 ambapo zinatolewa katika Kategori za Taaluma,Michezo,Utamaduni na Burudani na Mazingira na mambo ya kijamii ambapo wanavyuo waliweza kuwa na muda wa kuwachagua wenzao walioona kuwa walikuwa mstari wa mbele katika nyanja mojawapo kati ya hizo.
Baada ya kuwapata washindi sasa ni muda wa kuwapatia zawadi na tuzo zao ambapo zoezi hilo litafanyika katika viwanja vya TCC Club Chang”ombe siku ya jumamosi june 11,2011 kuanzia saa nne za asubuhi hadi saa kumi nambili na nusu jioni ambapo mgeni Rasmi ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Jordan Rugimbana.
Aidha Bi Edith Mushi amesema Kampuni ya Bia Tanzania itatoa jumla ya shilingi milioni 210 kama zawadi za fedha na vifaa mbalimbali.
Zawadi hizi zitatolewa kwa washindi wa nne wa kila nafasi yaani washindi wanne wa kwanza kwa kila chuo kupata kiasi cha shilingi laki nne(400,000.00), washindi wanne kila chuo walioshika nafasi ya pili watapata laki moja moja (100,000.00) na wengine wanne walioshika nafasi ya tatu kila chuo shilingi elfu hamsini(50,000.00). Aidha wanachuo wote walioingia katika hatua ya kumi bora katika kila kategori watapatiwa tuzo za vyeti maalum sambamba na tuzo kwaajili ya vyuo husika
Pia, wakati wa matamasha hayo kutakuwa na Burudani nyingi zitakazoongozwa na kundi la Wanaume TMK chini ya Temba na Chege, Joe Makini na Chid Benz ambapo pia burudani mchanganyiko toka katika vikundi mbalimbali toka vyuoni vitatoa burudani sambamba na michezo mbalimbali ikiwepo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba, mpira wa kikapu na meza.”Maandalizi kwa mikoa yote yamekamilika !
Kutakuwa na burudani nyingi nani wakati wa watanzaniua kufika kwa wingi katika viwanja vya TCC Club Chang”ombe na kushudia namna ambavyo wanachuo wanapata tuzo zao lakini pia kila ladha ya burudani itapatikana pale kwa siku hiyo ya jumamosi 11/06/2011 na hakutakuwa na kiingilio chochote na zaidi kutakuwa na usafiri wa kutoka vyuoni na kurudi vyuoni lakini pia hata wale ambao sii wanavyuo au wanavyuo ambao vyuo vyao havikushirikishwa kwa mwaka huu ni vyema wakaja kwa wingi ili kupata wasaa wa kuburudika na kukutana na wanavyuo wa vyuo vingine na kufurahi kwa pamoja.
Kwa mkoa wa Iringa, tamasha hili litafanyika siku ya jumapili ya june 12,2011 katika viwanja vya chuo kikuu Mkwawa, Mkoani Kilimanjaro ni June 18,2011 katika kiwanja cha chuo cha Ushirika (MUCOBS) na Mwanza ni june 19,2011 katika kiwanja cha Safisha uliopo katikati ya jiji la Mwanza na matamasha yote hayo yataanza saa nne kamili pasipo kuwepo na kiingilio chochote.


No comments:
Post a Comment