Mambo vipi Othman,
Ninakuletea Link hii
ambayo inahusu darasa la upigaji picha za movie (cinematography) litakaloendeswa na Barry Braveman kutoka California USA katika kipindi cha tamasha la kimataifa la filamu huko Zanzibar (ZIFF).
Tarehe za kujianndikisha ziko ukingoni, ninakuomba uwapatie taarifa wadau hususan filmmakers ili wachangamkie fursa hii adimu.
Richard.
NB:
Mwaka 2008 nilikutana na Barry katika mafunzo ya uandaaji wa filamu huko Kampala Uganda na alikuwa mwalimu wangu wa picha na mwanga (cinematography).
Nia yangu ya kutaka Barry aje Tanzania kuendesha darasa imefanikiwa baada ya kuwashawishi ZIFF wakisirikiana na TICA (Tanzania Independent Cinematographers Association).
No comments:
Post a Comment