Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania NAirobi, Bi. Grace Mgovano akijibu baadhi ya hoja zilizowasilishwa na wananchi wa Kenya waishio eneo la Namanga.
Kaimu Balozi akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Serikali ya Kenya ambaye pia ni Mbunge wa Eneo Bunge la Namanga, Kenya
Kaimu Balozi akiagana na Mh. Prof. Hellen Sambili, waziri wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Kenya baada ya kuhitimisha uzinduzi wa kituo hicho.
Sehemu ya Ujumbe wa Ubalozi wa Tanzania Nairobi ambao ulioshiriki katika uzinduzi huo
Kaimu Balozi wa Ubalozi wa Tanzania Nairobi, Kenya Bi. Grace Mgovano akishiriki katika uzinduzi wa Kituo Maalum cha kuhamasisha na kutatua kero mbalimbli za wananchi zinazijitokeza katika Nyanja mbalimbali ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Namanga.
Serikali ya Jamhuri ya Kenya kwa mara ya kwanza ilizindua Kituo hicho ambacho kitajulikana kama “Namanga Integration Centre”. Kituo hicho kilifunguliwa tarehe 17 Mei, 2011 na Mh. Prof. Hellen Sambili, Waziri wa Afrika ya Mashariki wa Jamhuri ya Kenya. Katika sherehe za uziduzi huo, Ubalozi wa Tanzania Nairobi uliwasilishwa na Kaimu Balozi Ms. Grace Mgovano.
Uzinduzi wa kituo hicho ni wa kwanza kufanyika ndani ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Uzinduzi wa kituo hicho ni sehemu ya Kampeni kabambe ya kitaifa yenye lengo la kuelimisha wananchi juu ya mchakato wa kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na urasimishaji wa soko la pamoja la Afrika ya Mashariki. Wizara pia inatarajia kufungua vituo vingine katika maeneo ya Busia, Malaba, Isebania, Lunga Lunga na Busia sambamba na utekelzaji wa Kampeni ya kitaifa ya siku 100 (Rapid Result Initiative) ambayo ilizinduliwa tarehe 24 Februari, 2011. Kituo cha Busia kinatarjiwa kuzinduliwa tarehe 24 Juni, 2011
Kimsingi vituo hivyo vinatarajia kutekelza majukumu yafuatayo:
(i) Kuwa na sehemu ya rejea katika masuala yote ya msingi juu mtangamano na urasimishaji wa Soko la Pamoja la Forodha ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(ii) Kusaidia kuweka mahusiano bora zaidi kati ya wadau mbalimbali wanaotumia mpaka wa Namanga na mipaka mingine;
(iii) Kuweka mtandao wa kimawasiliano katika eneo la mipakani;
(iv) Kuhakikisha uwepo wa upatikanaji wa taarifa muhimu kuhusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
(v) Kuwawezesha wananchi wa Kenya kunufaika ipasavyo na mtangamano huo; na
(vi) Kufuatilia kwa ukaribu utaratiu mzima wa kuondoa “non-tariff barriers”

No comments:
Post a Comment