HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 25, 2011

Kampuni ya Bia Tanzania TBL yaotesha miche 10,000 katika mji wa Moshi

Meya wa manispaa ya Moshi ,Mstahiki Jafary Michael akiongea na wananchi wakati wa maadhimisho ya siku ya ya upandaji miti katika manispaa ya Moshi .

Mgeni rasmi katika maadhimiso ya siku ya ya upandaji miti katika manispaa ya Moshi, Mkuu wa wilaya hiyo ,Musa Samizi akihutubia wananchi .

Meya wa manispaa ya Moshi ,Mstahiki Jafary Michael akiotesha mti.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya uoteshaji miti katika manispaa ya Moshi, Mkuu wa wilaya hiyo ,Musa Samizi akitosha mti katika eneo la Bomambuzi.
Meneja mawasiliano na uhusiano wa kampuni ya bia Tanzania(TBL)Edithi Mushi akiotesha mti.
Ivan Zarate raia wa Mexico aliyekuja nchini kwa ajili ya mchezo wa American footbal pia alipata fulsa ya kuotesha mti.
Kaimu meneja masoko wa TBL mkoa wa Kilimanjaro Edmund Rutaraka akiotesha mti wakati wa maadhimisho ya siku ya ya upandaji miti katika manispaa ya Moshi .
Wananchi na wafanyakazi wa manispaa pia walishiriki zoezi hilo.
Kina mama wakipanda miti katika eneo la Nagangamfumuni.
Meneja wa TBL kanda ya kaskazini Kasivo Msangi akiwaongoza wafanyakazi wa manispaa,wakiangalia maeneo yaliyopandwa miti kabla ya zoezi la uoteshaji miti kufanyika katika eneo la Bomambuzi.Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imechangia miche zaidi ya 10,000 kwa ajili ya kuotesha maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi ikiwa ni moja wapo ya kampeni za kupambana na ongezeko la joto katika mji wa Moshi.Picha na Dixon Busagaga,Moshi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad