HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 30, 2011

HALI SI SHWARI KWA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI TOSAMAGANGA MKOANI IRINGA HIVI SASA

Polisi wakiwaweka chini ya ulinzi wanafunzi eneo la Kitwiru nje kidogo na manispaa ya Iringa hapo ilikuwa ni kabla ya kuanza kupiga kurusha mabomu ya machozi.
Wanafunzi wa Sekondari ya Tosamaganga wakikimbia moshi ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na polisi
Mwandishi wa habari wa radio Ebony Fm akikimbia moshi ya mabomu ambayo yalikuwa yakipigwa na askari hao kutawanya wanafunzi hivi punde
Mwanakijiji kushoto akiwa na mwandishi wa habari wa Radio Ebony Fm wakifuta machozi kutokana na mabomu yaliyopigwa na askari hao kuwatawanya wanafunzi hao
Wengine wamaacha vitu vyao ili kuweza kujiokoa kwanza maisha yao.
Hapa wakikimbia porini kunusuru afya zao

Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 10000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao .

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .

Picha na Habari ni kwa Hisani ya Mdau Francis Godwin wa http://francisgodwin.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad