HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 6, 2011

TAASISI YA JOHNS UNIVERSITY YAANDAA MASHINDANO YA MPIRA WA MGUU KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI JIJINI ARUSHA

Na Mwandishi Wetu.

Taasisi ya Johns Hopkins University Center for Communication Programs kupitia mpango wa VOICES FOR MALARIA FREE FUTURE kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF,Benk ya NMB na kiwanda cha A to Z Textile Mills Limited kwa pamoja wataendesha kliniki ya watoto wa shule za msingi za mchezo wa mpira wa miguu na michezo hiyo itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha siku ya alhamisi ya Apri 7,2011.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Afisa Mradi wa Johns Hopkins bwana Furaha Kabuye alisema mashindano yatashirikisha watoto wadogo wenye umri wa kati ya miaka 8-10 na 10-12 kutoka kwenye shule za msingi nane za mkoa wa Arusha ambapo katika mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha zaidi ya watoto mia tano(500).

Bwana Kabuye alisema watoto hao watashiriki katika michezo ya mpira wa miguu kwa nyakati tofauti ambayo itakuwa imelenga kuadhimisha siku ya malaria duniani ambapo kwa mwaka huu kilele chake ni 25th April.

Barani Africa mtoto mmoja hupoteza maisha kila baada ya sekunde thelasini (30) kutokana na ugonjwa wa malaria ambapo pia malaria husabasha umasikini kwa jamii nzima kutokana na kuharibu nguvu kazi ya jamii husika, lakini malaria inawezekana kuzuilika na kutibiwa ikiwa sote kwa pamoja tutasema MALARIA HAIKUBALIKI.

Wote kwa pamoja tushirikiane kuutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kuunga mkono kauli mbiu ya serikali ya kushawishi kila mmoja wetu awe mwanamichezo,mabalozi wa malaria,makundi mbalimbali na mtu mmojammoja tuungane kwa pamoja kuhakikisha upatikanaji wa dawa za malaria na pia kuzingatia kinga dhidi ya malaria.

Mpira wa miguu unawashabiki wengi ulimwenguni hivyo basi wazazi na watoto wa hizi shule kwakushirikiana na wadau wengine wa kupinga malaria watashiriki katika kucheza mpira wa miguu.

Na sisi tunaamini mpira wa miguu una nafasi kubwa ya kufikisha ujumbe wetu wa kupiga vita ugonjwa hatari wa Malaria kwa jamii ya ya kitanzania .

Alisema Shule za msingi zitakazoshiriki katika mashindano haya ni pamojana; Sanawari, Mwangaza, Daraja, Meru, Levolosi, Engosengu, Unga and Makumbusho zote zikiwa ni za msingi na michezo hiyo itakuwa chini ya kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Jan Paulson.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad