HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 24, 2011

TAWLA kufanya kufanya mkutano na wanachama wake machi 26

Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) Maria Kashonda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar e salaam juu ya mkutano mkuu wa mwaka kwa wanachama wa TAWLA siku ya Jumamosi (26.3.2011) . Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa kimataifa wa Dar es salaam(DICC) juu ya uzinduzi wa kampeni ya uelimishaji jamii juu ya ushiriki wao katika mchakato wa kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wengine katika picha ni Mweka Hazina wa TAWLA Aisha Bade(kulia) na Mwenyekiti Mstaafu wa TAWLA na Wakili wa Kujitegemea Victoria Mandari(kushoto)
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano leo jijini Dar es salaam na uongozi wa Chama cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) . TAWLA inatarajia kuzindua kampeni ya uelimishaji jamii juu ya ushiriki wao katika mchakato wa kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumamosi 26.03.2011 jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad