HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 23, 2011

Prof. Mwandosya atembelea Mradi wa Maji TBL jijini Mwanza

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya (kulia) akitembelea Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Mwanza, alipofanya ziara hivi karibuni katika kiwanda hicho kuona uzalishaji wa bia na juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya Watu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.
Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Richmond Raymond (mbele kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya kutembelea mradi wa maji alipofanya ziara hivi karibuni kiwandani hapo, kujionea utendaji wa kiwanda hicho pamoja na mradi huo wa maji unaowahudumia bure wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad