
Jamaa wanaouza mayai ya kuku wakikata mitaa ya Kitunda mchana huu.

magari yanavyotumia barabara ya Kitunda

Wachuuzi wa mboga za majani a.k.a za kuongeza damu wakimwagilia maji mboga hizo ili zisinyauke kwa jua kali lililokuwa likiwaka.

Kitunda Relini.

Kitunda Stendi.

Njia ya kuelekea Mwanagati kutokea Kitunda.



Hii ndio Mwanagati kama inavyoonekana pichani.
Habari kaka Issa Michuzi! nimefurahishwa sana na taarifa na picha zinazohusu matukio ya eneo la kitunda mwanagati. kwa kifupi utoaji wa taarifa kama hizi ni changamoto ya maendeleo katika eneo husika ,si kitunda mwanagati peke yake hata maeneo mengine. ila kwa sasa katika eneo la kitinda mwanangat mtaa wa mzinga, kuna mto magole kwa upande wa nyuma, wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakisumbuka sana kipindi cha mvua na kuingiwa na hofu ya kupoteza makazi yao na kuhatarisha maisha ya watoto wao na afya kwa ujumla. maji yanayotiririka kutoka maeneo ya juu huishia kwenye makazi ya watu. eneo hili halina miamba chini kuweza kuzuia mmomonyoko na hivyo ni rahisi kuathiri makazi na miundo mbinu. serikali kwa miaka mingi sana imelifumbia macho suala hili na sasa linazidi kuwa kubwa kwani chemba za maji yanayoelekea mtoni zimeharibiwa kwa takriban miaka 7 na zaid bila kufanyiwa matengenezo jambo ambalo linasababisha maji kula pembezoni mwa mto kuelekeea makazi ya watu. inatia hofu zaidi kwani mkazi mmoja karibu na eneo hilo amekata barabara kuzuia maji yasielekee kwake na jufanya maji hayo kuleta athari kwa wakazi wa bondeni. ni hatari sana. kwa sababu natambua umuhimu wa vyombo vya habari katika mchango wa maendeleo ya taifa naomba ulifanyie kazi suala hili na hata kulifikisha panapostahili ili kuleta ahueni kwa wakazi hawa. ahsante sana.
ReplyDelete