
Salaam aleikum Wadau,
Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa Muumba wa Mbingu na Ardhi kwa kuweza kunifanikisha kiumbe chake mie kuwa hai mpaka leo hii na kufanikiwa kubadirisha namba katika umri wangu.
Kwani ni wengi wanapenda kufikikia hali hii lakini ni wachache wanaoweza kufikia hatua kama hii,hivyo yeye ndie anaestahiki pongezi nyingi huku dua nyingi tukiendelea kumuomba ili kutufakisha katika mlolongo mzima wa maisha.
Pili ni Wazazi wangu wawili walionizaa na kunilea katika malezi yaliyomema yenye kumuheshimu mkubwa na mdogo,wake kwa waume.
Tatu ni wale woote walioniwezesha kwa namna moja ama nyingine katika mlomlongo mzima wa maisha.Ninayo furaha kubwa sana kwa siku ya leo ambayo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu na pia kuwatakia sikukuu njema ya kuzaliwa wale woote waliozaliwa siku kama ya leo.na ninachoweza kuwaambia ni kwamba maisha ni mapambano na yatubidi tupambane kadri tuwezavyo ili kuhakikisha gurudumu hilo linasonga.
Nawashukuruni sana wadau wangu woote mnaonifuatilia kupitia libeneke langu hili la MTAA KWA MTAA kwani nyinyi pia ni sehemu ya maisha yangu ya kila siku na nawaahidi kutowaangusha kwa namna yeyote ile katika swala zima la matukio ya Mitaani popote pale nipitapo na kukuta kile ambacho nitaona kinafaa kuwemo katika list ya Libeneke letu hili.
Nasema Ahsanteni sana na Tuko PamoJah.

Nikifurahia Sikukuu yangu

Nikiwa katika moja ya Misele yangu ya Kazi.

Baada ya Kazi ni mapumziko ya kinamna namna kama hivi.

Pozz la Picha za sikukuu.

Nilipotembelea Shamba la Babu huko nanihii hivi karibuni.

Nikiwa na masela wa Mitaa ya kati wafanyao biashara ya Kuku wa Kienyeji pamoja na mayai yake.
Waaleykum salaam! Inshahlah Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema akutimize tamani njema za roho yako. Amina
ReplyDeleteKILA LAKHERI KATIKA MAISHA HAYA...NAMI NATANGULIZA SHUKRANI KWA MUNGU AKUPE MAISHA MEMA MENGI SIKU ZOTE.
ReplyDeleteTUPO PAMOJA DAIMA!
HAPPY BIRTHDAY.
Happy Birthday O! May God continue to bless you!!
ReplyDelete