HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 23, 2011

20% kutona na yanini malumbano

Msanii nyota katika muziki wa Bongo Flava aitwaye 20% , anatarajia kutambulisha albamu yake mpya inayoitwa "Yanini Malumbano" siku ya Jumapili wiki hii ndani ya ukumbi wa Club Maisha maeneo ya Oysterbay ,Kinondoni jijini Dar es Saalam.

Hayo yamesemwa leo hii jijini Dar es Saalam na mratibu wa uzinduzi huo Sigfred Kimasa a.k.a King Kif alipokuwa akizungumza na wanahabari.

Mratibu huyo amefafanua kwamba katika shoo ya uzinduzi wa albamu hiyo yenye nyimbo kumi,20% itasindikizwa na Man Water ambaye ndiye mtayarishaji wa albamu hiyo , Suleman Mshindi a.k.a Afande Selle kutoka mkoani Morogoro, Ney wa Mitego , Sajna, Linex na Uncle G.

Shoo imepangwa kuanza saa nne usiku na kuendelea hadi kuchee.

Kwenye albam hiyo ya Yanini Malumbano ndani yake kuna traki kali iitwayo Tamaa Mbaya ambayo kwa kipindi kidogo uumekuwa ukifanya vema katika vituo vya redio hapa Tanzania.

Traki zingine zilizomo kwenye albamu hiyo ni Neno la Mwisho, Nimerudi Salaama, Nyerere, Nia Yao, Mwema, Naficha, Kubadili Mwendo na Nimerudi Salaam.

Licha ya traki kali Yanini Malumbano kuvuma kwa sana katika vyombo vya habari hapa Tanzania ,albam hiyo imefanikiwa kufanya vema kwenye soko la muziki hapa Tanzania.

20% amewahi kutamba na albamu zake mbili miaka ya nyuma ambazo ni Money Money na Mama Neema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad