huu ni mtaro wa kupitisha maji na pia kuna kichaka kikubwa sana cha uchafu,kipo pale maeneo ya Mikocheni nyuma ya Majengo ya makao makuu ya Heinken,kiukweli ni pachafu kupitiliza pamoja na kwamba kijani kimetawala eneo hilo.wahusika kazi kwenu,maana mjumbe hauwawigi siku zote.
Cheki taka zilivyojikusanya sehemu moja.
Halafu wananchi tukilalamika kuwa hela yoyote ile inayoliwa na mafisadi inasababisha mambo kama haya, maana ebu fikiria hela ya RUSHWA, EPA, KIWIRA, TAX EXEMPTIONS, RADA, DOWANS, RICHMOND, MAGEREZA, NDEGE YA RAISI, TRA, KAGODA, MEREMETA, MASHANGINGI, BAJETI YA CHAI NA VITAFUNIO, ATCL, TANESCO, UFUJAJI WA MALIASILIZA TAIFA, BOT n.k.
ReplyDeleteKama hela zote hizo zingetumika kwenye miundo mbinu, kununua magari ya fire na kuboresha jeshi la zimamoto, sidhani kama tungekua na majanga kama haya.
Hela yoyote inayoibiwa serikalini lazima utapata upungufu kwenye maisha ya mwananchi wa kawaida.
Ila kila tukilalamika hatusikilizwi na CCM bado wanapigiwa kura tu kuendeleza mambo kama haya.