
Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr.Norman Sigalla wa pili toka kushoto akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10 na Benki ya KCB Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lyasikika ya wilayani mwake,kushoto kwake Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa benki hiyo Christina Manyenye,kulia kwake Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Dr.Edmund Mndolwa,Mkuu wa Idara ya mikopo Ronald Kitti.

Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Dr.Edmund Mndolwa(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr.Norman Sigalla hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lyasikika ya wilayani humo,wapili toka kushoto Mkurugenzi wa masoko na uhusiano wa benki hiyo Christina Manyenye,Mkuu wa kitengo cha mikopo Ronald Kitti,Hafla hii ilifanyika katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dares Salaam leo.
No comments:
Post a Comment