HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 10, 2010

utamaduni unanafsi kubwa ya kuleta maendeleo nchini - UNESCO


Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kanda ya Afrika limesema kuwa sekta ya utamaduni ina nafasi kubwa ya kusaidia kuleta maendeleo na kupunguza umaskini kwa wananchi ikiwa itaijumuishwa kikamilifu katika mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mshauri wa masuala ya Utamadani wa UNESCO kanda ya Afrika Bibi Moji Okuribido wakati akitoa mada kuhusu nguvu ya utamaduni katika kuleta maendeleo.

Bibi Okuribido alisema kuwa ni vema wapangaji mipango wakakuchukua maoni ya jamii husika na utamaduni wao wakati wakiandaa miradi mbalimbali kabla ya kuanza kuitekeleza ili suala la utamaduni wa sehumu husika hapa baadaye usiwe kikwazo katika utekelezaji kwa jamii.

"Ni vema wakati wa kutekeleza miradi kusikiliza mtazamo wa jamii kuliko kuamua mambo ambayo wakati mwingine yanakwamishwa kwa kuwa hayaendani na utamaduni wa eneo husika" alisisitiza mshauri huyo wa UNESCO.

Aliongeza kuwa suala la utamaduni linapaswa kuwa kiungo katika mipango ya maendeleo kwa kuwekeza kwa muda mrefu kwa sekta hiyo ikiwemo kuweka miundombinu inayosaidia kukua kwa utamaduni nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Malikale, Ndugu Donatius Kamamba alitoa wito kwa sekta mbalimbali kuangalia tathmini ya athari za utamaduni kabla ya kuanzisha miradi ili kufanya inapoanzishwa iungwe mkono na jamii kwani itakuwa imetokana na mtazamo na taratibu za utamaduni husika.

Alisema kuwa baadhi ya miradi na mipango imeshindwa kudumu kwa kuwa suala la utamaduni halikupewa kipaumbele kabla ya uanzishwaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad