
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa,Nahodha wa timu ya Taifa ya Pool,Aliakber A. Aliakber ambao wanataraji kuondoka leo usiku kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo.katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager ambao ndio wadhamini wakuu wa mchezo huo hapa nchini,Fimbo Buttallah.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana (katikati) akizungumza machache katika hafla fupi ya kuiaga timu ya Taifa ya Pool inayotaraji kuondoka nchini leo usiku kuelekea nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Dunia ya mchezo huo,katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya Inter Grated,iliopo Kinondoni Moroco. kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh. Jordan Rugimbana akiwa matika mazungumzo ya furaha na Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Bullallah mara baada ya hafla ya kuiga timu ya Taifa ya Pool inayokwenda nchini Ufaransa kushiriki mashindano ya Dunia.katikati yao ni Afisa Habari wa Kampuni ya Inter Grated,Innocent Melleck.

Kocha wa timu ya Taifa ya Pool,Dennis Lungu akiwa na vijana wake katika hafla ya kuagwa kwao leo.
No comments:
Post a Comment