HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 9, 2010

kikosi cha kilimanjaro stars chatangazwa leo

Kocha mkuu wa timu ya Taifa,Jan Poulsen (pili kulia) akitangaza kikosi ya timu ya Kilimanjaro Stars leo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka nchini (TFF).wengine pichani ni Katibu Mkuu wa TFF,Sunday Kayuni (kulia),Meneja wa bia ya Tusker,Nandi Mwiyombella (pili shoto) na kushoto ni Afisa Uhusiano wa SBL,Imani Lwinga

*************************
Mwandishi Wetu
KOCHA wa timu ya taifa Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 22 huku akimrudisha kundini  mshambuliaji Gaudence Mwaikimba na Juma Nyosso ambao walitemwa kwa kipindi kirefu katika kikosi cha Mbrazil Marcio Maximo.

Mwaikimba mshambuliaji wa zamani wa Yanga alikuwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Stars chini ya Kocha, Marcio Maximo raia wa Brazil, hata hivyo baadaye alimuacha mshambuliaji huyo kutokana na kushuka kiwango na baadae kufungashiwa virago na Yanga.

Hata hivyo mchezaji huyo ambaye awali alikuwa kipenzi cha Maximo kutokana na umbile lake amekuwa lulu kwenye timu ya Kagera anayochezea hivi sasa na aliweza kumshawishi Poulsen amrudishe kundini baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi uliomalizika mwishoni mwa wiki.

Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars ambacho kitashiriki michuano ya Chalenji iliyopangwa kuanza Novemba 27 hapa nchini ni mlinda mlango Juma Kaseja (Simba), Shaban Kado (Mtibwa) na Said Mohamed wa Majimaji.

Wengine ni Shedrack Nsajigwa, Erasto Nyoni, Stephano Mwasika, Shamte Ally, Idrisa Rajabu, Shaban Nditi, Henry Joseph (Kongsvinger- Norway), Nurdin Bakari, Jabir Aziz, Nizar Khalfan (Vancouver Whitecapes -Canada), Salum Machaku, Mohamed Banka na Kiggi Makasi.

Wengine ni Dan Mrwanda (DT Long - Vertinam), Mrisho Ngasa, John Boko, na Thomsa Ulimwengu anayesakata soka la kulipwa nchini Sweden.

Akitangaza kikosi hicho Poulsen alisema baadhi ya wachezaji hao pia wataunda kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kitakachocheza mechi ya taifa ya kirafiki Novemba 17 kujiandaa na michuano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika baadae mwakani itakayofanyika Gunea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad