HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 5, 2010

Hussein Bashe ndani ya Radio Mbao Wiki hii

Kama tunavyojua mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi. Vimbwanga na vionjo vya uchaguzi havikuanza katika zoezi la kupiga kura, bali pia vilianza hata wakati wa kura za maoni.

 Miongoni mwa wagombea na kijana aliejitokeza kugombania nafasi ya uwakilishi wa wananchi Bungeni alikuwa ni Hussein Bashe, ambaye alikuwa na nia ya kugombea ubunge wa jimbo la Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 Kama tunavyoelewa,Hussein hakupitishwa kugombea nafasi hiyo kwa sababu ya madai ya kutokuwa raia wa Tanzania.

Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Hussein Bashe kujua yaliyojiri kwenye mchakato wa kuteua wagombea wa ubunge, mipango yake siku za usoni, mtazamo wake juu ya mustakhabali wa taifa la Tanzania na mengine mengi.

Jiunge nasi kwa kupitia hapa: 


 ili usikose uhondo!


Utawala
Radio Mbao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad