
Marehemu Syllersaid Mziray
MAKAMU Mkuu WA Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly S.A. Mbwette, Na Menejimenti yote ya Chuo, anasikitika kutangaza kifo cha Mkufunzi Wa Michezo, Syllersaid Mziray.
Mziray alifariki dunia alfajiri ya kuamkia leo Jumamosi katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa amelazwa kwa karibu wiki mbili kutokana na Malaria na baadaye matatizo ya figo.
Taratibu za Mazishi zinaendelea nyumbani kwake Tabata Magengeni. Mziray atazikwa Jumatatu kwenye Makaburi ya Kinondoni. Mazishi hayo yatatanguliwa na utoaji wa heshima hapa chuoni.
Mungu ailaze roho ya marehemu Syllersaid Mziray Pema Peponi Amen!
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO NA MASOKO,
CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA,
S.L.P. 23409,
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment