HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 17, 2010

ARUSHA MAMBO YAIUNGANISHA MITANDAO MINNE YA SIMU KATIKA HUDUMA YAKE YA HABARI NA MATANGAZO KWA NJIA YA MESEJI


Mmiliki wa Arusha Mambo Bw, Elifuraha Paul Mtowe akisisitiza jambo alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari wa Luninga na Magazeti kuhusina na uhakika wa utoaji wa Habari za Dharura na Matangazo ya Kampeni na Sera za Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wakati huu wa uchanguzi Mkuu kwenda kwenye simu za Mkononi kwa wakazi wa Kanda ya Kaskazini ya Tanzania.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Arusha Mambo Bi. Rosemerry William (mwenye koti Jeusi) akiwa ametembele Fine Food Supermarket iliyopo Njiro Arusha, kushuhudia shamrashara za uzinduzi wa Kampuni ya Arusha Mambo.
Bi. Rosemerry William (mwenye koti Jeusi) akiwa amewatembelea wafanyakazi wa Ukumbi wa Sinema wa Kisasa wa Cinemas uliopo katika Jengo la Njiro Complex, kushuhudia shamrashara za uzinduzi wa Kampuni ya Arusha Mambo.
Hapa ndipo panapochomwa Nyama ya Mbuzi yenye Kiwango cha hali ya juu Arusha Nzima ‘’Qx Pub Kijenge’’ wanaonekana wafanyakazi wa Qx Pub wakiwa katika pilikapilika za uzinduzi wa Mpango wa habari na matangazo kwa Njia ya Meseji kupitia Arusha Mambo.
Watu wenye usafiri watafaidika na kujiunga katika huduma ya Arusha Mambo kwani licha ya kupata Habari na Matangazo pia mteja wa 3000 kujiunga atapata lita 50 za mafuta kutoka hapa Engen Petrol Station – Arusha
Mbele ya Vibanda vinne vya Kampuni za Vodacom, Zain, Tigo na Zantel inaonekana Wananchi wa Arusha wakikimbilia kupata maelezo ya huduma mpya ya Habari na Matangazo kwa njia ya Ujumbe mfupi wa Simu yaliyokuwa yanatolewa na vijana wa Arusha mambo katika Promosheni ya uzinduzi wa huduma hiyo.

******* ******* *******

Kampuni Mpya ya Arusha Mambo iliyoanza hivi karibuni Mjini Arusha, imefungua biashara yake ya kwanza ya kutuma Habari na Matangazo kwa njia ya ujumbe mfupi kwa wateja wa mitandao minne mikubwa ya Simu hapa nchini Tanzania.

Wafanyabiasha ambao wamekuwa kwa muda mrefu wakilalamikia gharama za matangazo ya biashara; sasa watapata nafuu kubwa wakati wa kutangaza biashara na bidhaa zao kufuatia huduma mpya ya kutuma matangazo ya biashara moja kwa moja yakiwa katika mfumo wa Ujumbe mfupi kwenda kwa wamiliki wa simu za mkononi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Arusha Mambo Bw. Elifuraha Paul Mtowe wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo amewaambia waandishi wa habari kuwa, licha ya malalamiko ya muda mferu ya gharama kubwa wanazoingia watangazaji kwa kutumia njia zilizozoeleka za kutangaza za Luninga, Redio, Vipeperushi, Mabango, Nguo na Magari ya Matangazo Barabarani bado aina hiyo ya kutangaza imekuwa haiwafikii walengwa na imekuwa na muitikio mdogo wa asilimia mbili tu kwa soko lililokusudiwa.

Amesema kwa mtangazaji kutangaza kwa kutumia Ujumbe mfupi, atakuwa na hakika ya kuwapata wateja wake kwa asilimia 95%, popote walipo na kwa wakati wowote na kuna hakika ya kupata muitikio kwa asilimia 25% ya soko lililokusudiwa kwani uchunguzi unaonyesha asilimia 94% ya meseji zote zinazotumwa husomwa katika kipindi cha dakika nne tu toka zilipotumwa, aidha amesema hiyo ni mara tano zaidi ya watu wanaosoma matangazo katika barua pepe, mara tisa zaidi ya watu wanaosoma vipeperushi na matangazo mengine ya karatasi na mara 69 zaidi ya watu wanaosoma matangazo katika magazeti.

Bwana Mtowe amesema, kwa kuwa imethibitika kuwa watu wengi wana simu za mkononi kuliko simu za mezani na watu wengi wanauwezo wa kupata huduma ya simu za mkononi kuliko barua pepe na mtandao; wakati umefika sasa wa kukiongezea chombo hicho maana ili kitumike kumnufaisha mtangangazaji na mlaji katika soko la Kitanzania.

Amesema ili kujiunga mmiliki wa simu wa kati ya mtandao wa Vodacom, Zein, Tigo na Zantel, aliyepo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, atatakiwa kutuma neno arushamambo kwenda nambari 15522. Aliongeza kuwa, kwa kujiunga na huduma hii itakayokuwa inaangalia Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Tanzania ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara na Singida mteja huyo atakuwa pia amejihakikishia kupata habari za Dharura zitakazotumwa moja kwa moja katika simu yake ya Mkononi ikiwa ni pamoja na habari mbalimbali za Sera na Matangazo ya Kampeni wakati huu tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu.

Mkurugenzi huyo amesema, wateja 6000 wa mwanzo kujiunga katika huduma hii watapata zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuingia Sinema katika Ukumbi wa Kisasa wa Sinema wa Cinemas – Njiro, Muda wa maongezi wa Shilingi 50,000 kutoka Arusha Mambo, Lita 50 za mafuta kutoka Engen Petrol Station – Ilboru, Kuponi ya Bidhaa kutoka Fine Food Supermarket – Njiro, Kulala usiku mmoja katika Hotel ya Kitalii ya Snow Crest Arusha, HD Media Player kutoka Sound & Vision, Kuponi ya Shilingi 50,000/= ya vinywaji na Nyama ya Mbuzi yenye Kiwango kutoka Qx Pub – Kijenge na mteja wa 6000 kujiunga atapewa zawadi ya Simu aina ya Blackberry 8520 kutoka Arusha Mambo.

Amesema kwa mawasilano zaidi, wateja wanaweza kuwasiliana nao kwa barua pepe info@arushamambo.com au info@arushapamoja.com au kwa kupiga Simu Namba +255 764 444444 na au kwa kutuma meseji tu kwenda nambari +255 763 123000 – Arusha.

2 comments:

  1. Kwa mtego mdogokama huu! Hutupati kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
    But kila la kheri

    ReplyDelete
  2. hongera sana mtumishi wa bwana.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad