
Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa Mawasiliano ya Mambo ya NJe wa Tigo. Alex Kamara akimkabidhi Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala mchanganuo wa mradi wa ushirikiano katika kuongeza ugunduzi wa tatizo la mtoto wa jicho kwa watoto na pia kutoa mafunzo kwa wakunga

Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa Mawasiliano ya Mambo ya NJe wa Tigo.Alex Kamara akifafanua zaidi kuhusu ushirikiano wao na taasisi ya CCBRT ,waliouanzisha katika kuongeza ugunduzi wa tatizo la mtoto wa jicho kwa watoto na pia kutoa mafunzo kwa wakunga, ikiwemo pia na ufadhili wao wa kliniki za macho ambazo hutoa huduma za uchunguzi na tiba ya matatizo ya macho kwa watoto hasa tatizo la mtoto wa jicho zinazofanyika mara mbili kwa mwaka mkoani Mwanza.Kliniki ya kwanza ya macho kwa watoto itafanyika tarehe 8 hadi tarehe 19 Novemba 2010 na ya pili itafanyika Julai 2010. Tigo pia itafadhili mafunzo ya wiki mbili ya kozi ya huduma za uzazi (BEmONC) kwa wakunga 10.
Mkurugenzi Msaidizi wa CCBRT Haika Mawala ambaye alisema kuwa asilimia 80 ya upofu unaweza kuzuiwa kupitia kwa matibabu au kuzuia na ni muhimu kuwafikia watoto wengi iwezekanavyo,waliozaliwa na mtoto wa jicho nchini Tanzania. "Ninafurahi kuwa Tigo inatambua kazi ya kubadilisha maisha ambayo CCBRT inafanya katika jamii hapa jijini Dar na kwingineko."alisema Haika na kuongeza kuwa kupitia ushirika huo ambao ni muhimu sana mkoani Mwanza, Watoto wapatao 160 ambao wangepata upofu watapata kuona na hivyo kuweza kuishi maisha mema zaidi. (Habari na picha kwa hisani ya Cathbert Kajuna).
No comments:
Post a Comment