Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng akihutubia jana jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa chemsha bongo kuhusu miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China. Shindano hilo liliendeshwa kwa ushirikiano wa Radio China Kimataifa(CRI) , Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) , Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ).
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Clement Mshana (kulia) akihutubia wakati wa sherehe fupi ya utoaji wa tuzo kwa washindi wa chemsha bongo kuhusu miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China leo jijini Dar. Kushoto ni Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China ya Kimataifa (CRI). Shindano hilo liliendeshwa kwa ushirikiano wa Radio China Kimataifa(CRI) , Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) , Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ).
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando akimpatia leo jijini Dar mmoja wa washindi wa tuzo ya shindano la chemsha bongo kuhusu miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na China , Bwana Adison Gamba(kulia). Shindano hilo liliendeshwa kwa ushirikiano wa Radio China Kimataifa(CRI) , Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) , Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ).Picha na Tiganya Vincent - MAELEZO
No comments:
Post a Comment