
Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania, Joram Kiarie akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, Tiba Kalufya na Mayasa Hemed mara baada ya kuikabidhi shule hiyo msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu. Kulia ni mkuu wa idara ya masoko na mahusiano wa benki hiyo Christina Manyenye.

Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim, mara baada ya hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo na samani za ofisini kwa ajili ya walimu vyenye thamani ya Milioni 4/- ili kusaidia kupunguza uhaba wa vifaa unaoikabili pamoja na kuinua kiwango cha elimu iliyofanyika shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment