HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 27, 2010

HOSPITALI YA REGENCY KUJENGA KITUO KIPYA CHA AFYA

Daktari Bingwa wa tiba za Mifupa, viuongo na upasuaji kutoka India Kaushal Mishra akizungumza na waandishi wa habari juu ya namna atakavyofanya kazi kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Regeny.
Mwenyekiti wa Hospitali ya Regency Dr. Rajni Kanabar (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya uimarishaji na utoaji wa huduma za magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya mifupa na viungo, moyo, figo na magonjwa ya mfumo wa njia ya mkojo kwa kushirikiana na mataktari bingwa kutoka nchini India leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni meneja wa mifumo ya komyuta ya hospitali hiyo Jingne Oza.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na Mwandishi Wetu.

UONGOZI wa Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam ,umesema unajenga kituo kikubwa cha afya kwa ajili ya kutoa huduma za afya chenye thamani ya dola za Marekani milioni 15 ili kupunguza gharama za wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa hospitali hiyo, Dk. Rajni Kanabar wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ushirikiano wao wa kutoa tiba mbalimbali na kundi la madaktari bingwa kutoka India (Forts – Hospital Health Care Limited).

“Tumepata eneo jingine kwa ajili ya ujenzi wa kituo kikubwa katika eneo lililojirani na hospitali yetu, ambapo tunajenga mahabara ya kisasa na vyumba vya upasuaji viwili, sehemu ya huduma ya dharura na uongozi. Hivyo tumeshaanza ujenzi huo lengo ni kupunguza gharama kwa Watanzania kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya tiba mbalimbali,”

alisema.

Dk. Kanabar alisema ujenzi huuo untarajia kuchuku kipindi cha miaka miwili.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano wa madaktari hao kutoka India, Dk. Kanabar alisema watakuwepo hapa nchini kwa kipindi cha miezi mitatu kwa ajili ya kutoa tiba na ushauri kwa wagonjwa ikiwemo kutoa mafunzo kwa madaktari wa hapa nchini, hata hivyo aliongeza baada ya muda huo kumalizika watakuja wengine.

Alisema uzinduzi rasmi wa ushirikiano huo, utazinduliwa Oktoba 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Madaktari hao, ni Dk. Rajesh KR. Pandit ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya moyo na Dk. Avinash Ingnatuius mtaalamu wa magonjwa ya figo ambao waliwataka Watanzania kufika hospitalini mapema ili kufanya matibabu kuwa rahisi badala ya kusubiri hadi wazidiwe.

Wengine ni Dk. Kushaul Mishra ambaye ni mtaalamu wa mifupa na viungo alisema wamefurahishwa kuja Tanzania. ambapo lengo lao ni kutoa ujuzi kwa madaktari waliopo nchini hususan namna ya kufanya upasuaji mgumu na Dk. Aman Gupta mtalaamu wa magonjwa yanatokana na mfumo wa njia ya haja ndogo.

Madaktari hao watatoa tiba hizo kwa gharama nafuu na kufanya upasuaji mdogo.

“Tutatumia kifaa kidogo kwa ajili ya kugundua matatizo ya mfumo wa haja ndogo ambacho hakiko Tanzania,” alisema Dk Gupta.

Hopitali ya Regency imetoa ufadhili kwa watoto zaidi ya 1,000 kwaa ajili ya upasuaji wa moyo kwa gharama ya dola za Marekani 1,650 hadi 2000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad