kamera ya Mtaa kwa Mtaa ilimnasa mtoto huyu maeneo ya morocco jijini dar,akiosha kioo cha moja ya magari yaliyokuwa yamesimama kusubiri ruhusa ya taa za kuongozea magari.wengi wa watoto hawa ambao wapo katika maeneo mengi ya jiji la dar,wameamua kujishughulisha na kazi hii ili kuweza kujipatia kipato kutoka kwa wamiliki wa magaro hayo.
hawa nao kazi yao ni kusimama katika vibaraza vilivyopo katikati ya barabara na kuendelea kuomba huku wazazi wao wakiwa wamekaa pembeni tena kivulini kabisa wakisubiria hela zitakazipelekwa na watoto hawa.sijui ni juhudi gani zifanyike ili kuweza kulitokomeza kabisa swala hili la hawa watoto kuka humu mabarabarani??.
No comments:
Post a Comment