HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 30, 2010

Wabunifu kutoka Tanzania kutafuta soko Uingereza

Baadhi ya wabunifu waliofika katika mafunzo ya Swahili Fashion week wakisikiliza kwa makini pindi mafunzo hayo yalipokuwa yakitolewa.


**************************************************
Wabunifu wa mavazi 12 wanapata mafunzo yaliyoandaliwa na Swahili Fashion Week kwa kushirikiana na Tanzania Cotton Board (TCB) na Textile Sector Development Unit (TSDU) yenye lengo la kuboresha taaluma ya ubunifu wa mavazi hapa nchini.

“kwa siku ya kwanza tu nimejifunza mengi, natarajia kupata mengi zaidi katika masula mazima ya kuboresha kazi yangu na jinsi ya kutafuta masoko ya ndani na nje”. Alisema Salim Ally mbunifu wa mavazi anayechipikia katika fani hasa kwa upande wa mavazi ya vijana katika mtindo unaojulikana kama la Mtoko wear.

Miongoni mwa wabunifu waliopata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo ni pamoja na Kemi Kalikawe, Margherita Marvassi kutoka Zanzibar , Jamila Vera Swai, Zamda George, Francisca Shirima, Farha Sultan, Ailinda Sawe, Manju Msita, Salim Ally, Kim Dean, Rabi Morro na Angelo Elly Mlaki.

“Tunaamini kwamba mafunzo haya yatawawezesha wabunifu wa watanzania kuweweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitaweza kuuzwa sehemu yoyote. Pia kupitia mafunzo haya tunaamini kwamba wabunifu watapata habari muhimu zitakazowawezesha kuchangia moja kwa moja ukuaji wa sekta ya ubunifu Tanzania”. Alisema Mustafa Hassanali muaandaji wa Swahili Fashion Week.

Mafunzo hayo ya siku nne yanaendeshwa na Claire Hamer-Stubbs ambae anatoka katika kampuni ya Ei8ht (www.ei8ht.org), kundi ambalo limekuwa likifanya kazi zake nchini Uingereza, na yanafanyika katika hoteli ya New Africa.

Textile Sector Development Unit (TSDU) kwa sasa inashirikiana na Swahili Fashion Week katika programu ya kuwasaidia wabunifu wa Tanzania kwa kutoa mafunzo ya awali , TSDU inaamini kwamba kwa kutoa fursa ya mafunzo kwa wabunifu ambayo yatawawezesha kutambua mpangilio mzima wa kufanya kazi zao kwa ubora zaidi. Pia inaamini kwamba kupitia semina hii wabunifu watajipatia uelewa mpana wa kufanya kazi na wanunuzi wa rejareja kutoka Uingereza ambao huenda wakavutiwa na bidhaa zinazozalishwa na wabunifu wa Tanzania.

KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK

Swahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Swahili fashion week in tukio ambalo linawajumuisha wabunifu wakongwe na wale wanaochipukia kuonyesha kazi zao, pia kutoa nafasi kwa wapenzi wote wa sanaa ya mavazi kujumuika pamoja na kufurahia bunifu wa watanzani na kutoka nchi za jirani.

Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.

Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika kuanzia tarehe 4 mpaka 6 November 2010, Dar Es Salaam, Tanzania.

KUHUSU UKUAJI WA VIWANDA (TSDU)

The Tanzania Cotton Board’s (TCB) na Textile Sector Development Unit’s (TSDU) zimekua zikisaidia kukuza seka ya viwanda Tanzania. Lengo kuu ni kubuni hali bora na kuhakikisha kukua viwanda vinavyozalisha nguo Tanzania, sambamba na kuhakikisha thamani ya Pamba Tanzania inakua, hali itakayochangia kupatikana kwa nafasi za ajira na kuwepo kwa hali bora kwa nchi ya Tanzania.

KUHUSU TANZANIA GATSBY TRUST (TGT)

The Tanzania Gatsby Trust (TGT - www.gatsby.or.tz) imeanzisha program maalumu ya kusaidia serikali ya Tanzania katika kuhakikisha maendeleo ya viwanda vinavozalisha nguo . miongoni mwa program zake nyingi pia ni kusaidia kukuza hali ya wabunifu wa Tanzania. TGT inaamini kuwa kuimarika kwa sekta ya ubunifu kutachangia kuongezeka kwa ajira Tanzania. Kwa kushirikian ana VETA TGT imeanzisha mafunzo ya wabunifu wa maonyesho katika vituo vyake vya mafunzo vilivyopo Dar es salaam. Pia TGT imeamua kufanya kazi na Swahili Fashion Week kwa lengo kukuza hali ya ubunifu wa mavazi Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad