
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Leonidas .T. Gama akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Tawi jipya la huduma kwa wateja la kampuni ya simu za mkononi la Tigo lililofunguliwa leo mtaa wa msimabzi na Pemba. Kushoto kwake anaeshuhudia ni Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez . wakati wa ufunguzi wa tawi hilo jipya mtaa wa kariakoo pia Tigo ilitangaza kufungwa rasmi kwa promosheni yao iliyoendeshwa kwa miezi mitatu ya JIKOKI na Tigo.

Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Leonidas .T. Gama mapema leo asubuhi jijini Dar.

Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez akimueleze akizungumza na vyombo vya habari mbalimbali mapema leo kuhusiana na hafla fupi ya ufunguzi Rasmi wa tawi hilo jipya la huduma kwa wateja lililofunguliwa leo mtaa wa msimabazi na Pemba.

Pichani ni Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Leonidas .T. Gama jinsi walivyoboresha ofisi zao za huduma kwa wateja kwa kuweka mashine maalum zakukusanyia maoni ya wateja (Customer feedback system) ili waweze kuziboresha huduma zaidi muda mfupi baada ya hafla fupi ya ufunguzi Rasmi wa Tawi hilo jipya la huduma kwa wateja lililofunguliwa leo mtaa wa msimabazi na Pemba.

Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Leonidas .T. Gama akipokea zawadi kifurushi cha huduma zinazotolewa na Tigotoka kwa mmoja wa Afisa wa Tigo huduma kwa wateja Beatrice Kinabo ikiwa ni maalum kwa kumpongeza mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Tawi jipya la huduma kwa wateja la kampuni ya simu za mkononi Tigo lililofunguliwa leo mtaa wa msimabazi na Pemba. Kushoto mwa Beatrice ni Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez .
No comments:
Post a Comment