
Lil Kim na densa wake wakilishambulia jukwaa

Juma Nature akijiachia na Lil Kim jukwaani katika fiesta jipanguse usiku wa kuamkia leo.

Lil Kim baada ya kupiga songi zake kadhaa,alimuita msanii Juma Nature jukwaani na kuanza kuimba nae,ama kwa hakika kuliibuka makelele na mayowe ya shangwe ile mbaya katika viwanja vya lidaz klabu usiku wa kuamkia leo.

watu kibao walijiachia katika fiesta jipanguse usiku wa kuamkia leo ndani ya viwanja vya lidaz klabu.

Lil Kim na densa wake wakionesha umahiri wao wa kucheza na jukwaa mbele ya mashabiki waliofika katika viwanja vya lidaz klabu kujipangusa ki fiesta.

Wasanii kutoka nchini Nigeria,Smash na Vast wanaounda kundi la Bracket wakilishambulia jukwaa usiku wa kuamkia leo katika fiesta jipanguse.

Kikosi cha aldji aladji jukwaani kikitumbuiza.

Mkali wa aladji aladji kutoka Ivory Coast,Jeff akimchezesha densa wake na kibao chake maarufu kabisa cha aladji mbele ya umati mkubwa uliofika kwenye tamasha la fiesta jipanguse ndani ya viwanja vya lidaz club.

Kundi la Wanaume TMK,Chege,Themba na Kr Mulla wakilivamia jukwaa vyema kabisa na moja ya wimbo wao wa Mambo bado.

Msanii Mataluma kutoka THT na wimbo wake wa Mama Mubaya

Mwasiti akiimba wimbo wake wa Kisa Pombe.

Wasanii mahiri kutoka THT,Barnaba na Lina wakilivamia jukwaa huku wakiwa wamezungukwa na baadhi ya madensa,ama kwa haki fiesta jipanguse hapa dar imenoga ile mbaya,shangwe kila kona zilitawala.

full nyomi lidaz club

Msanii wa THT na wimbo wake wa robo saa akiimba jukwaani na madensa wake

Wasanii kutoka THT wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaani ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,viwanja vya Lidaz Club kinondoni jijini Dar.

Wwoooowwwww..!

Ni shangwe miluzi na makelele kwa kwenda mbele.
kwa picha zaidi jibonyezee
No comments:
Post a Comment