HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 9, 2010

FAINALI ZA MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KANDA YA ZIWA

Kundi la Kakau kutoka mkoani Kagera likiwajibika ipasavyo katika mashindano hayo,kundi hili ndilo lililoibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyokuwa yakiendele jijini Mwanza.
Kundi la "Mang'ombe ya Kijiji" toka Missungwi nao hawakuwa nyuma kuonyesha cheche zao,hawa waliambulia kupata nafasi ya Tatu ya mashindano hayo ya ngoma za asili yalikuwa yakifanyika ndani ya uwanja wa Nyamagana,jijiniMwanza.
Kundi la Bujora ambao walishika nafasi ya pili ya mashindano hayo.
Kundi La Kakau likiwa katika picha ya pamoja baada ya kutwaa Ubingwa


Mashidano ya ngoma za asili katika kanda ya ziwa yanayodhaminiwa na bia ya BALIMI EXTRA LAGER jana yamefikia tamati katika uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza na Kundi la ngoma toka Kagera - KAKAU GROUP wameibuka na ushindi wa kwanza. Kundi la Kakau ndilo lililokuwa likishikilia nafasi hiyo baada ya kuongoza katika mashidano ya mwaka jana.

Mashindano ya ngoma za asili kwa kanda ya ziwa 2010, yalianza tarehe 17 Julai 2010 na kushirikisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Tabora katika ngazi ya mikoa na vikundi viwili vilyoshika nafasi za juu kila mkoa viliingia katika fainali kuu ya kanda iliyofanyika August 7 jijini Mwanza.

Lengo la mashindano haya yanayodhaminiwa na TBL kupitia bia ya BALIMI EXTRA LAGER ni kuenzi na kudumisha mila desturi za makabila ya kanda ya Ziwa, na pia kuongeza mshikamano wa makabila haya kupitia utamaduni wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad